MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA MAJI IKUNGI AMBAO UTAWANUFAISHA WANANCHI 2,628

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu (kushoto), Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi wakifurahia mara baada ya Makamu wa Rais kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha  Uliyampiti ambapo mradi huo wa maji utawahudumia wakazi 2628.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Uliyampti tayari kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628. Makamu wa Rais yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku tano ambapo atakagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628.
Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AIPONGEZA MAHAKAMA NA WADAU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Rais  Dkt. John  Magufuli ameipongeza Mahakama na wadau wake kwa hatua kubwa za kimaendeleo zilizopigwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *