VITUO VYA AFYA 350 VITAKUWA VIMEKAMILIKA NCHI NZIMA NDANI YA MIAKA TANO

  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema vituo vya afya 350 vitakuwa vimekamilika nchi nzima ndani ya miaka mitano ya Uongozi wa Awamu ya tano
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Migori wilayani Singida.
  • Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati alipotembelea kituo cha afya cha Sokoine wilayani ya Singida mkoa wa Singida ikiwa muendelezo wa ziara yake ya kikazi ambapo amekuwa akikagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
  • “Kulikuwa na hospitali 65 za wilaya lakini tulivyoingia madarakani zimejengwa hospitali 67 na lengo kuu ni kuwapa wananchi huduma bora ya afya” alisema Makamu wa Rais.
UJENZI-5
Naibu Waziri Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa barbara ya Karume iliyopo Singida mjini ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ndio alikuwa mgeni rasmi.
  • Aidha Makamu wa Rais alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitokubalina na misaada ya masharti na imejidhatiti kufanya miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha zake za ndani.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Migori wilayani Singida kutoka kwa Kaimu Mhandisi wa Wilaya Dayness Rwehumbiza. Kituo cha afya cha Migori ni moja ya vituo vilivyopata shilingi milioni 400 za kitanzania.
  • Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alizindua barabara ya Karume ambayo inajumuisha mradi wa mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 6.1 ambazo nibarabara ya Karume yenyewe , Boma Kinyeto, Double Road Junction (Semali Singida-Dodoma ).
Wanafunzi wa Shule
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori wilayani Singida wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yupo ziarani mkoani Singida.
  • Sambamba na hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea kituo cha afya Migori ambapo alijionea maendeleo ya ujenzi ambao unatazamiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi machi, pia alitembelea shule ya sekondari ya Mwanamema Shein ambapo alizungumza na wanafunzi na kujionea maendeleo ya ujenzi wa bweni la wanafunzi pamoja na kupanda mti wa kumbukumbu.
Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye mti wa kumbukumbu alioupanda katika shule ya sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori wilayani Singida.
  • Wakati huo huo Naibu Waziri wa maji ameahidi kutoa tanki la maji la lita 10,000 kwa ajili ya kituo cha afya cha Karume ikiwa kama jitihada za kumuunga mkono Makamu wa Rais ambaye amejitoa kuhakikisha afya ya mama na mtoto inakuwa salama.
JIWE LA MRADI
Jiwe la Mradi
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI UMMY AWATAKA WAZAZI KUWEKEZA KATIKA AFYA ZA WATOTO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wazazi kuwekeza …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *