SERIKALI YAKUTANA NA WAZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA YA PLASTIKI NA WADAU WA BIASHARA YA TAKA HATARISHI NCHINI

MAKAMBA
Sehemu ya wazalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki kutoka Kampuni mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia Serikali kuwa wako tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote nchini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini ifikapo tarehe 1 Juni 2019.
JANUARY
Bw. Heneriko Batamuzi kutoka Kampuni ya Kenwood Enterprise (T) Ltd akichangia mada katika kikao cha wadau cha kupitia Rasimu ya Kanuni za kusimamia Taka Hatarishi hapa nchini. Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa rasimu ya Kanuni mpya za kusimamia Taka Hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na ukusanyaji, urejelezaji, uteketezaji na usafirishaji wake ndani na nje ya nchi. Kikao hiki kimefanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA AFRIKA MASHARIKI SALAMA KWA MAZINGIRA – WAZIRI ZUNGU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.