WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AKUTANA NA WAWEKEZAJI TOKA UTURUKI

BS
Wafanyabiashara wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Viwanda akiwaeleza kuhusu faida za kuwekeza nchini
  • Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amekutana na ujumbe wa wafanyabiashara toka nchini Uturuki katika ofisi za Kiuo cha Uwekezaji (TIC). Ujumbe huo ulioongozwa na balozi wa Uturuki nchini Mheshimiwa Ali Davutaglu ulihusisha wafanyabiashara wa sekta za ujenzi, utalii, chakula na viwanda mbalimbali.
BS
Balozi wa Uturuki akimkabidhi Waziri wa Viwanda zawadi ya mojawapo ya bidhaa zinazotengenezwa Uturuki kwa niaba ya ujumbe wa wafanyabiashara
  • Wafanyabiashara hao walielezea sifa ya Tanzania kuwa na amani kama kivutio cha wao kutaka kuwekeza nchini na kusema wangependa kufungua ofisi itakayokuwa kiungo baina ya wafanyabishara wa Uturuki na wale wa Tanzania.
BS
Mheshimiwa Innocent Bashungwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara pamoja na balozi wa Uturuki
  • Mheshimiwa Bashungwa amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba Tanzania ni nchi salama na yenye mazingira rafiki kwa wawekezaji akiahidi kuhakikisha Wizara ya Viwanda na Biashara ikishirikiana kwa ukaribu na taasisi nyingine za Serikali itaharakisha taratibu zote zinazotakiwa ili waanze uwekezaji wao mapema iwezekanavyo. Pia aliahidi kuwakutanisha na wafanyabiashara wengine nchini ili wapate kufahamiana na kubadilishana ujuzi.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KAIRUKI AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *