MABORESHO YA MFUMO WA HAKI JINAI YAHAKIKISHE WANANCHI WANAPATA HAKI – LUGOLA

  • Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Kangi Lugola amekitembelea  kikosi kazi kinachopitia mfumo wa haki jinai nchini ili kuufanyia maboresho na kukitaka kuangalia kwa umakini maeneo yote ambayo yamekuwa changamoto na kuwafanya wananchi kukosa haki zao.
LG 1-01
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akimpokea Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola alipowasili katika hoteli ya St. Gasper jijini Dodoma kukitembelea kikosi kazi kinachofanya mapitio ya mfumo wa haki jinai nchini na kuzungumza nacho.
  • Mhe. Lugola ametoa kauli hiyo alipotembelea kambi maalum ya wataalamu wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo iko jijini Dodoma kwa ajili ya kuupitia mfumo wa haki jinai nchini na kuangalia changamoto inazoukabili mfumo huo ili kuufanyia maboresho.
  • “Nimekuja hapa kuangalia kazi mnayoifanya ila nataka niwaambie kwamba muangalie kwa makini maeneo yote katika mfumo wa haki jinai ambayo yamekuwa yakiwanyima haki wananchi na hata kufanya haki za binadamu kuvunjwa,” amesema
LG
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola alipowasili katika hoteli ya St. Gasper jijini Dodoma kukitembelea kikosi kazi kinachofanya mapitio ya mfumo wa haki jinai nchini na kuzungumza nacho.
  • Mhe. Lugola amewataka wataalamu wanaofanya kazi hiyo ya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini kuangalia namna ya mashauri yanayoweza kupata dhamana, muda wa kuendesha mashauri ya watuhumiwa na aina za adhabu zinazotolewa ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati kwani haki inayocheleweshwa ni sawa na kunyimwa haki.
  • Pia amewataka kuangalia, namna ya kukabiliana na rushwa kubwa na mabadiliko ya sayansi na teknolijia ambayo yamesababisha kuongezeka kwa mbinu za uhalifu na hivyo kuuacha nyuma mfumo wa haki jinai nchini.
  • Amesema wazo la kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai litawezesha mfumo huo kwenda na wakati na kutoa haki kwa wananchi huku haki za binadamu zikizingatiwa.
LG 3-01
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola kuhusu kazi ya maboresho ya mfumo wa haki jinai inayofanywa na kikosi kazi maalum jijini Dodoma ambapo mhe. Waziri aliwatembelea na kuzungumza nao.
  • Ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kukutanisha wadau mbalimbali kutoka serikalini na nje ya serikali ili kufanya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini na kumtaka Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome kufikisha salamu kwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga kwa kuja na mpango wa kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai nchini na kwamba kitendo hicho ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala cha CCM .
  • “Katibu Mkuu niwapongeze sana na nikuombe umfikishie salamu za pongezi mhe Waziri Dkt. Mahiga, kitendo cha kuufanyia maboresho mfumo wa haki jinai ni cha kupongezwa, kimekuja wakati na kinatekeleza kwa vitendo ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020,” amesema.
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *