Maktaba ya Mwezi: February 2020

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA AFRIKA MASHARIKI SALAMA KWA MAZINGIRA – WAZIRI ZUNGU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu hii leo ameshuhudia makabidhiano ya Cheti cha tathmini ya athari kwa mazingira kwa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la afrika mashariki ikiwa ni hitimisho la ripoti ya Tathmini ya mazingira kwa Mradi wa …

Soma zaidi »

MAFINGA WAKABIDHIWA RASMI MAJENGO YALIYOPO KATA YA CHANGARAWE ILI KUYATUMIA KUWA KITUO CHA AFYA

  Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amesema kuwa wameakabidhiwa rasmi majengo  yaliyopo katika Kata ya Changarawe,  ambayo yalikuwa yakitumiwa na Mkandarasi wa barabara ya Mafinga – Igawa ili yatumike Kama Kituo cha Afya. Mbunge huyo alitoa maombi ya kukabidhiwa majengo hayo kwa Rais Dkt. John Magufuli  wakati akitokea katika …

Soma zaidi »

MOI YALETA MITAMBO YA KISASA YA UPASUAJI UBONGO BILA KUFUNGUA FUVU

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kwa dhati kuboresha Sekta ya Afya nchini na tayari imeleta mitambo ya kisasa ya Maabara ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite). Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Taasisi …

Soma zaidi »

SERIKALI MKOANI SHINYANGA YAKUSANYA  BILIOINI 1.5 KAMA KODI YA MRABAHA NA ADA YA UKAGUZI KUTOKA KWA WACHIMBAJI

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph kumburu amesema kuwa utaratibu mzuri uliowekwa kwenye usimamizi wa uzalishaji na biashara ya madini kwa wachimbaji wasio rasmi mkoani Shinyanga umepelekea Serikali kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.56 kama kodi ya mrabaha na ada ya ukaguzi kuanzia mwezi Mei, 2019 hadi …

Soma zaidi »

RAIS MAGUFULI AIPONGEZA MAHAKAMA NA WADAU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Rais  Dkt. John  Magufuli ameipongeza Mahakama na wadau wake kwa hatua kubwa za kimaendeleo zilizopigwa katika kipindi cha miaka 4 iliyopita na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha Mahakama inaboreshwa zaidi. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo tarehe 06 Februari, 2020 katika sherehe za kilele cha Wiki ya Elimu na Siku ya …

Soma zaidi »

TRA – WAFANYABIASHARA MSIJIHUSISHE NA BIASHARA ZA MAGENDO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara na wachuuzi wanaoishi jirani na fukwe za Bahari ya Hindi kutojihusisha na biashara za magengo kwani kufanya hivyo ni kuisababishia nchi kukosa mapato yake stahiki kutokana na wahusika wa biashara hizo kukwepa kulipa kodi. Akizungumza na wafanyabiashara hao katika fukwe za bahari za …

Soma zaidi »

ZANZIBAR NA ANGOLA KUSHIRIKIANA KWENYE SEKTA YA UTALII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameupongeza uwamuzi wa busara na wenye tija wa Angola wa kutaka kushirikiana na Zanzibar kwenye sekta ya utalii hatua ambayo itaimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo. Dk. Shein aliyasema hayo leo, Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na …

Soma zaidi »