Maktaba ya Mwezi: February 2020

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zinatakiwa kujitazama na kushauriana kuhusu mwenendo wao wa uchumi badala ya kuyaachia Mashirika ya Kimataifa pekee. Rai hiyo imetolewa Jijini Dodoma wakati wa …

Soma zaidi »

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI SADC, BALOZI WA EU NA BALOZI WA CHINA

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Februari, 2020 amekutana na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Manfred Fanti na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke, Ikulu Jijini Dar es Salaam. …

Soma zaidi »

KATIBU MKUU DKT. ABBASI ASISITIZA MAGEUZI YA KIUTENDAJI KWA MENEJIMENTI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi amewataka viongozi wa menejimenti wa Wizara hiyo kufanya mageuzi kwa kuwa sekta za wizara  hiyo zimebeba ushawishi mkubwa kwa nchi  na dunia. Dkt.Abbasi ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma baada kuwasili katika ofisi ya wizara hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba …

Soma zaidi »

BILIONI 8 KUJENGA MAABARA YA KISASA YA UCHUNGUZI MAGONJWA AMBUKIZI HOSPITALI YA KIBONGO’OTO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni Nane (8) kwa ajili ya ujenzi wa Maabara kubwa na ya kisasa ya uchunguzi wa magonjwa ambukizi ikiwemo ya Kifua Kikuu katika Hospitali maalum ya Magonjwa ya kuambukiza Kibong’oto, mkoani hapa. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa …

Soma zaidi »

TUNAWEKA MIKAKATI YA KUPANDA MITI ZAIDI YA MILIONI 1 KATIKA MLIMA KILIMANJARO – WAZIRI ZUNGU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema Serikali inatarajia kuweka mikakati ya kupanda miti zaidi ya milioni moja kwenye eneo la Mlima Kilimanjaro ili kulinda barafu iliyopo nchini. Pia amewataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti na kuitumia kama fursa ya …

Soma zaidi »

WAKAZI WA PEMBEZONI MWA BAHARI WAELIMISHWA ATHARI ZA MAGENDO

Wakazi na wafanyabiashara waishio pembezoni mwa fukwe za Bahari ya Hindi katika kata za Somangila, Kimbiji na Pemba Mnazi zilizopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wameelimishwa kuhusu athari za magendo yanayopitishwa kinyume na sheria katika maeneo hayo. Elimu hiyo imetolewa wakati wa kampeni maalum ya kuelimisha wananchi kuhusu …

Soma zaidi »

WAZIRI UMMY AKAGUA JNIA TERMINAL 3 UTAYARI WATUMISHI WA AFYA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameridhishwa na hali ya ukaguzi wa abiria wanaoingia nchini katika uwanja wa ndege wa Kimataifa cha Julius Nyerere(JNIA) jengo la tatu la abiria-TB3 dhidi ya homa kali ya mafua inayoenezwa na virusi vya Corona. Awali akiwa uwanjani hapo aliweza …

Soma zaidi »

NENDENI MKATANGULIZE UZALENDO KWANZA – RAIS MAGUFULI

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi walioapishwa kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za uongozi pamoja na kuwa na   hofu ya Mungu bila kusahau kutanguliza Uzalendo katika kuhakikisha Tanzania inafikia malengo iliyojiwekea. Rais Magufuli Ameyasema hayo leo tarehe 3 Februari 2020 katika hafla ya Uapisho wa Viongozi mbalimbali …

Soma zaidi »

DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI KATIKA WILAYA YA KINONDONI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na kusababisha athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo. Vibali vilivyositishwa katika ni vile vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde la …

Soma zaidi »