TANAPA YATAKIWA KUONGEZA IDADI YA MABANGO YA TAHADHARI BARABARANI ILI KUPUNGUZA IDADI YA WANYAMAPORI WANAOGONGWA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akizungumza katika mkutano uliowakutanisha kwa pamoja Wadau wa Uhifadhi kujadili jinsi ya kulinda shoroba ya Kwakuchinja pamoja na maeneo mengine muhimu ya Wanyamapori  katika  ikolojia ya Tarangire na  Manyara katika mkutano uliofanyika katika wilaya ya Babati mkoani Manyara. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu na kushoto ni Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  Constantine  Kanyasu ametoa agizo kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuongeza idadi ya mabango ya barabarani  yanayoonyesha tahadhari na  faini kwa madereva watakaogonga wanyamapori katika barabara ya Babati kuelekea Arusha.


Ametoa agizo hilo katika wilaya ya  Babati mkoani Manyara katika mkutano wa Wadau wa Uhifadhi uliowakutanisha Wataalamu mbalimbali kujadili namna ya kulinda mapito asili ya wanyamapori    (shoroba) pamoja na maeneo mengine muhimu ya wanyamapori ambayo yapo hatarini kutoweka kufuatia kushamiri kwa shughuli za kibinadamu Kanyasu amesema kukosekana kwa tahadhari hizo kunatishia kuharibika kwa ikolojia ya Tarangire na Manyara kutokana na idadi kubwa ya wanyamapori kuuawa kwa kugongwa na magari kila siku.

Ad


Kwa mujibu wa takwimu jumla ya wanyamapori 588 wakiwemo simba na twiga waliuawa mwaka jana kwa kugongwa na magari yanayopita kwa spidi katika barabara hiyo

Kufuatia hali hiyo,  Mhe.Kanyasu ameitaka TANAPA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanyamapori ya Burunge kukutana na Uongozi wa TANROAD ili waweze kutekeleza agizo hilo la uongezaji mabango katika barabara hiyo.  

Akizungumzia mazimio ya Mkutano huo, Mhe. Kanyasu amemuagiza  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuunda kikosi kazi cha wataalamu mbalimbali kwa ushirikiano wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Babati kutambua mipaka ya shoroba katika   vijiji

Mbali na maazimio hayo, Mhe, Kanyasu amemtaka Mkuu wa wilaya ya Babati  Kuhakikisha maeneo ambayo tayari yanatambulika kuwa ni shoroba yalindwe ili yasiendelee kuvamiwa.

Aidha, Mhe.Kanyasu amemtaka Mkuu wa wilaya ya Babati kuhakikisha anatoa maagizo kwa  Uongozi wa  vijiji vinavyozunguka shoroba hawagawi maeneo ambayo ni  shoroba  kwa  Wananchi kwa ajili ya shughuli za kibinadamu ikiwemo ujenzi na kilimo.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *