RAIS MAGUFULI – WATANZANIA WOTE TUENDELEA KUDUMISHA AMANI AMBAYO NI MUHIMU KWA MAENDELEO YETU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia zawadi ya viatu alivyokabidhiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee (kushoto) baada ya kufungua rasmi kiwanda cha kisasa cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kabla ya kukifungua rasmi eneo la Karanga mjini Moshi Alhamisi Oktoba 22, 2020  .

Rais Dkt. John Magufuli tarehe 22 Oktoba, 2020 amezindua kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd) kilichojengwa katika eneo la Gereza Kuu la Karanga, Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa ubia wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF) na Jeshi la Magereza Tanzania.

Mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho umehusisha uboreshaji wa kiwanda cha zamani kilichojengwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere mwaka 1978 kwa ajili ya kuzalisha viatu vya kijeshi ambapo kilikuwa kikizalisha jozi 150 kwa siku, na sasa kimeboreshwa na kuongeza uzalishaji hadi kufikia viatu 400 kwa siku.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua bidhaa za Ngozi pamoja na mashine za Kiwanda hicho cha Ngozi cha Kilimanjaro International leather Industries Co Ltd kilichojengwa kwenye eneo la Gereza Kuu la Karanga mkoani Kilimanjaro tarehe 22 Oktoba 2020.

Kiwanda kipya na cha teknolojia ya kisasa kilichowekezwa hivi sasa na ambacho kimeanza uzalishaji kina uwezo wa kuzalisha jozi Milioni 1.2 za viatu kwa mwaka, soli za viatu jozi milioni 2.1 kwa mwaka pamoja na bidhaa mbalimbali za Ngozi kama vile mikanda, mabegi, pochi na makoti, na pia kitakuwa na uwezo wa kuchakata futi Milioni 13 za ngozi ambazo kwa asilimia 60 zitatumika kiwandani hapo na asilimia 40 kuuzwa ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Hosea Kashimba amesema uwekezaji wa kiwanda hicho umegharimu shilingi Bilioni 136, kinatarajiwa kutoa ajira takribani 3,000 za moja kwa na 7,000 zisizo za moja kwa moja, na kwamba katika kujihakikishia upatikanaji wa malighafi za uhakika PSSSF inashirikiana na wadau wengine kuwekeza katika machinjio ya kisasa nchini ili kupata ngozi bora za kukilisha kiwanda hicho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua bidhaa za Ngozi pamoja na mashine za Kiwanda hicho cha Ngozi cha Kilimanjaro International leather Industries Co Ltd kilichojengwa kwenye eneo la Gereza Kuu la Karanga mkoani Kilimanjaro tarehe 22 Oktoba 2020.

Baada ya kuzindua kiwanda hicho, Mhe. Rais Magufuli amejionea jinsi vijana wa Kitanzania wanavyofanya kazi kwa kutumia mitambo ya kisasa ya kutengeneza viatu bora vya aina mbalimbali na pia amenunua jozi kadhaa za viatu vilivyokuwa tayari kwa kuuzwa.

Akizungumza na wananchi waliohudhuria tukio hilo,  Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na kukamilika kwa kiwanda hicho ambacho kimeboreshwa na kuwekezwa mitambo na majengo mapya kwa maelekezo yake, na amesema anaamini uzalishaji wake utaendelea kupanuliwa ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza viatu nje ya nchi ambapo takwimu zinaonesha Tanzania inaagiza jozi Milioni 52 za viatu kwa mwaka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua bidhaa za Ngozi pamoja na mashine za Kiwanda hicho cha Ngozi cha Kilimanjaro International leather Industries Co Ltd kilichojengwa kwenye eneo la Gereza Kuu la Karanga mkoani Kilimanjaro tarehe 22 Oktoba 2020.

Rais Magufuli amesema pamoja na ajira za moja kwa moja zitakazozalishwa na kiwanda hicho, ajira nyingine takribani Milioni 3 zitazalishwa kutokana na mnyororo wa thamani, soko la ngozi litapanuliwa na hivyo ametoa wito kwa wafugaji kuzalisha ngozi bora.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro International leather Industries Co Ltd kilichojengwa kwenye eneo la Gereza Kuu la Karanga Moshi mkoani Kilimanjaro tarehe 22 Oktoba 2020.

Ameipongeza PSSSF yenye asilimia 86 ya hisa za kiwanda hicho na Jeshi la Magereza kwa kufanikisha uwekezaji huo, na ametoa wito kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na wadau wengine kuendelea kuwekeza katika viwanda kama ambavyo wamefanya katika miaka mitano iliyopita ambapo Tanzania imefanikiwa kujenga viwanda vipya 8,470.

Wafanyakazi mbalimbali wa Kiwanda hicho cha Ngozi cha Kilimanjaro International leather Industries Co Ltd wakiwa wanatengeneza viatu vya aina mbalimbali mara baada ya uzinduzi wa Kiwanda hicho.

Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kuendelea kudumisha amani ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda, hasa wakati huu ambapo Tanzania imeingia katika uchumi wa kati, na amesisitiza kuwa Serikali itahakikisha inaendelea kujenga mazingira bora ya uwekezaji ili Watanzania wanufaike.

Wafanyakazi mbalimbali wa Kiwanda hicho cha Ngozi cha Kilimanjaro International leather Industries Co Ltd wakiwa wanatengeneza viatu vya aina mbalimbali mara baada ya uzinduzi wa Kiwanda hicho.
Wafanyakazi mbalimbali wa Kiwanda hicho cha Ngozi cha Kilimanjaro International leather Industries Co Ltd wakiwa wanatengeneza viatu vya aina mbalimbali mara baada ya uzinduzi wa Kiwanda hicho.

Sherehe ya uzinduzi wa kiwanda hicho imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Jenister Mhagama, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira, viongozi wa Dini, viongozi na watendaji wakuu wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kufungua rasmi kiwanda cha bidhaa za Ngozi pamoja na mashine za Kiwanda hicho cha Ngozi cha Kilimanjaro International leather Industries Co Ltd kilichojengwa kwenye eneo la Gereza Kuu la Karanga mkoani Kilimanjaro tarehe 22 Oktoba 2020.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MWENDO KASI LEOTakwimu za Sasa za Utekelezaji wa Mradi wa Mwendo Kasi kwa Mwaka 2024

Mradi wa Mwendo Kasi (BRT) nchini Tanzania unaendelea kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wake mwaka …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *