SERIKALI KUIIMARISHA TRC KWA KUNUNUA MABEHEWA MENGINE 800 YA MIZIGO, 37 YA ABIRIA NA VICHWA 39 VYA TRENI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Arusha na Kilimanjaro akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020.

Rais Dkt. John Magufuli leo tarehe 24 Oktoba, 2020 amezindua safari za treni ya abiria kati ya Dar es Salaam Tanga na Arusha ambazo zilisimama zaidi ya miaka 30 iliyopita.

Uzinduzi wa safari hizo umefanyika Jijini Arusha ambapo Mhe. Rais Magufuli amepokea treni ya abiria iliyotoka Jijini Dar es Salaam na kupita katika reli iliyokarabatiwa na wataalamu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Arusha mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020.

Ukarabati wa reli hiyo umeanza Desemba 2019 na kukamilika Septemba 2020 kwa gharama ya shilingi Bilioni 14 kwa kutumia wataalamu na vijana wa Tanzania, na tayari treni imeshasafirisha abiria 50,576 na zaidi ya tani 26,000 za mizigo.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja Kadogosa amesema kuanza kwa safari za treni kati ya Dar es Salaam, Tanga na Arusha kumepunguza gharama za usafiri ambapo nauli ya abiria kati ya Dar es Salaam na Arusha ni shilingi 16,000 ikilinganishwa na shilingi 35,000 inayotozwa kwa usafiri wa mabasi, ilihali usafirishaji wa mizigo kwa tani ni shilingi 68,000 ikilinganishwa na shilingi 110,000 kwa kutumia malori.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa viongozi wa TRC mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020.

Bw. Kadogosa ameongeza kuwa pamoja kurejesha usafiri wa treni wa kati ya Dar es Salaam, Tanga na Arusha, TRC inaishukuru Serikali kwa kuiwezesha kukarabati mabehewa ya mizigo 600 ambapo mabehewa 333 yamekamilika, kuunda vichwa vya treni vipya 23, kununua vichwa vipya 11 na kwamba shirika hilo limetenga eneo Jijini Arusha kwa ajili ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuweka eneo la kuhifadhi makontena ili wananchi wapokee mizigo yao ya kutoka nje ya nchi moja kwa moja Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Arusha mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua moja ya behewa la abiria mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020.

Pia ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge) kati Dar es Salaam na Dodoma ambapo sehemu ya kwanza ya kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro ujenzi umefikia asilimia 90 na sehemu ya pili ya kuanzia Morogoro hadi Makutupora Dodoma ujenzi umefikia asilimia 45.3.

Rais Magufuli ameipongeza TRC kwa kazi nzuri iliyofanya kukarabati miundombinu ya reli, mabehewa na vichwa vya treni na ameeleza kuwa mafanikio hayo yamedhihirisha kuwa Watanzania wanaweza bila kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi ama kampuni za nje ya nchi kuendesha mashirika ya Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Arusha kabla ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuzungumza na wananchi wa Arusha kabla ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020.

Rais Magufuli amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja Kadogosa na bodi ya TRC kwa usimamizi mzuri wa shirika hilo ambalo lilionekana kupoteza mwelekeo na sasa linakuwa kimbilio la Watanzania na tegemeo la kujenga uchumi wa nchi.

Amesema kwa kutambua umuhimu wa reli, Serikali imedhamiria kuiimarisha TRC ambapo katika mwaka ujao imepanga kununua mabehewa mengine 800 ya mizigo, 37 ya abiria na vichwa 39 vya treni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kuzungumza na wananchi wa Arusha kabla ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Arusha akiwa juu ya treni ya Abiria mara baada ya kuzindua huduma ya usafiri wa Treni ya Abiria ya Shirika la Reli TRC kutoka Dar es Salaam hadi Arusha katika hafla fupi iliyofanyika katika Stesheni ya Arusha leo tarehe 24 Oktoba 2020.

Ametoa wito kwa Watanzania kutoihujumu miundombinu ya reli na badala yake washirikiane na TRC na vyombo vya dola kuilinda isiibiwe ama kuharibiwa.

Sherehe za uzinduzi huo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kwandikwa, Makatibu Wakuu, viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Bw. Idd Hassan Kimanta.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *