WABUNGE WAMPONGEZA KASSIM MAJALIWA KUPITISHWA JINA LAKE KUCHAGULIWA KUWA WAZIRI MUU

Aliyekuwa Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackoson, ameshinda tena nafasi hiyo kwa kupata kura 350 kati ya Kura 354 zilizopigwa.
Naibu Spika wa bunge la 12 Dk.Tulia Ackson kupitia CCM akiwashukuru wabunge waliomchagua kwa kishindo wakati wa Bunge la 12 Jijini Dodoma leo tarehe 12 Novemba 2020
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kuwashukuru Wabunge baada ya kumthibitishwa na Bunge kwa kupigiwa kura na kupata kura 350 sawa na asilimia 100 kutoka kwa wabunge wote ambapo hakupata kura ya hapana.

Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Job Ndugai akisaini karatasi yenye jina la kupendekezwa Waziri Mkuu baada ya kupokea kutoka kwa mpambe wa Rais,ambapo Rais Dkt John Magufuli alipendekeza jina la Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipiga kura kumchangua Waziri Mkuu, wakati wa kikao cha tatu Bunge la 12 kilichofanyika katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, jana. (Picha na Muhidin Sufiani)
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimpongeza Mbunge wa Jimbo lwa Ruagwa, Majaliwa Kassim Majaliwa, baada ya jina lake kuteuliwa kupigiwa kura ya kuchaguliwa na Wabunge kuwa Waziri Mkuu, wakati wa kikao cha tatu Bunge la 12 kilichofanyika katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, jana. (Picha na Muhidin Sufiani)
Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *