WAWEKEZAJI WAZAWA WAJITOSA KATIKA UCHUMI WA BLUU

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Abdallah Hussein Kombo amesema endapo Zanzibar itajikita zaidi kwenye uchumi wa buluu kupitia shughuli za uvuvi visiwani hapa utasaidia kukuza ajira na kukuza uchumi wa Zanzibar.

Jana Waziri huyo alitekeleza miongoni mwa maagizo aliyoyatoa Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi kuhusu kukutana na wadau wa sekta ya uvuvi wakiwemo kampuni ya uvuvi ya Salmini,wavuvi na benki ya Equity.

Ad

Akizungumza katika uzinduzi wa uvuvi na mikopo kwa wavuvi uliondaliwa na benki hiyo ya Equity

Waziri huyo alisema serikali ya awamu ya  nane imeamua kujikita kwenye uchumi wa bluu  ambapo tayari imeonyesha ishara nzuri mpaka sasa.

“Kampuni ya uvuvi ya Salmini imepata soko la samaki aina ya jodari nchini Finland,Uturuki na  China ambapo kila mwezi wanatakiwa samaki tani 5,000 hivyo kampuni hiyo imepanga kununua samaki kwa wavuvi wadogo visiwani Zanzibar,”alisema

Waziri huyo alisema licha ya kuwepo kwa  fursa hiyo pia benki ya Equity imejionyesha utayari wake wa kutoa mikopo kwa wavuvi kutoa mikopo ya zana za kisasa za uvuvi.

“Mimi ninaomba kampuni za uvuvi ikiwemo Salmini,wavuvi na benki ya Equity kushirikiana kwa pamoja kupitia kamati za wavuvi zilizopo vijijini ili kutimiza azma ya serikali kupitia uchumi wa buluu,”alisema

Katika maelezo yake alisema serikali ya Zanzibar ya awamu ya nane imeamua kujikita kwenye uchumi wa buluu kupitia sekta ya uvuvi ili kukuza ajira, kukuza uchumi wa Zanzibar.

“Zanzibar ina wavuvi zaidi ya 50,000 hivyo kuna haja wadau wa sekta ya uvuvi kukutana na kamati  za uvuvi ili kuona namna ya kunufaika na uchumi wa buluu ambao unajumlisha pia suala la ufugaji wa samaki na si uvuvi tu pekee yake,”alisema

Waziri huyo alisema kuna haja ya kuona wadau hao wanakutana mara kwa mara ili kuharakisha suala la upatikanaji wa fedha katika miradi mbalimbali ya sekta ya uvuvi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Equity Robert Kiboti alisema tayari wamejipanga katika kuwawezesha wavuvi wadogo kunufaika kupitia uchumi wa buluu.

Alisema benki hiyo ipo tayari kuunga mkono  kipaumbele cha serikali ya Zanzibar ya uchumi wa buluu kwa kuwapatia mikopo wavuvi ikiwemo mikopo ya zana za kisasa za uvuvi.

“Benki yetu ipo tayari kuwafikia wavuvi wote  katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar ili  kuwawezesha wavuvi kufikia malengo yao na kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko chanya katika uchumi wa buluu,”alisema

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya uvuvi ya Salmini Dk.Salmin Ibrahim Salmin alisema tayari kampuni hiyo imewaunganisha vikundi vidogo vya wavuvi wapatao 3500 kwa ajili ya kupata fursa ya sekta hiyo.

“Tumeona tuwaunganishe wavuvi hao kutokana na  kuwa wavuvi wanahitaji mitego ya kisasa,soko la uwakika,wanahitaji mikopo,zana bora,bandari ya uvuvi,viwanda vya kusindika samaki hivyo tuliona umuhimu wa kuwaunganisha,”alisema

Alisema kupitia kampuni hiyo tayari wamefanya mazungumzo na muwekezaji kutoka Uturuki kwa ajili ya kuwekeza bandari ya uvuvi na kiwanda cha  kusindika samaki ambacho kitagharimu  dola za kimarekani bilioni 3.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdory Mpango, tarehe 01 Novemba 2024 ameungana na kuongoza Waombolezaji Katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo,jijini Dar-es-Salaam, kuaga mwili wa marehemu Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *