Taarifa ya Habari

MAWAZIRI WA NISHATI WA AFRIKA MASHARIKI WAAHIRISHA MKUTANO WAO

Mawaziri wenye dhamana na sekta ya nishati kutoka nchi sita zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameahirisha Mkutano wao uliopangwa kufanyika Arusha, Juni 7 mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa EAC anayeshughulikia Sekta ya Uzalishaji, Jean Baptiste Havugimana, ilieleza kuwa Mkutano huo utafanyika siku nyingine katika tarehe itakayobainishwa na …

Soma zaidi »

RAIS MAGUFULI AMFUTA MACHOZI MFANYABIASHARA ALIYEZUILIWA BIDHAA ZAKE TANGU 2015

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kumlipa fidia mfanyabiashara ambaye bidhaa zake zilishikiliwa na Mamlaka hiyo tangu mwaka 2015 kinyume na taratibu. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Juni 7, 2019 wakati akiongea na wafanyabiashara kutoka wilaya …

Soma zaidi »

SERIKALI YAKABIDHI MFUMO WA USIMAMIZI WA MASHAURI OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI

Serikali Kupitia Wakala ya Mtandao (e GA) imekabidhi rasmi Mfumo wa Taarifa wa Usimamizi Mashauri, kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kuiwezesha Ofisi hiyo Kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi Mkubwa. Akizungumza ya Waandishi wa Habari katika makabidhiano kati ya Wakala ya Serikali ya Mtandao na Ofisi ya Wakili …

Soma zaidi »

WATANZANIA WANAOISHI UK KUFANYA HARAMBEE YA KUNUNUA JENGO LA JUMUIYA

Jumuiya ya Watanzania UNITED KINGDOM -TZUK DIASPORA itafanya uzinduzi wa harambee na kampeni kubwa ya ununuzi wa jengo la kisasa kwa ajili ya jumuiya Jengo hilo linategemewa kuwa na kila aina ya huduma za kijamii na kuitangaza Tanzania nje ya nchi Akizungumzia kampeni hiyo hivi karibuni Mwenyekiti wa Jumuiya ya …

Soma zaidi »

TATIZO LA MAJI NANDAGALA LAWA HISTORIA

Wananchi washangilia, waishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma CHANGAMOTO ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama iliyokuwa inawakabili wananchi wa vijiji vya Nandagala ‘B’ na Ingawali wilayani Ruangwa imekuwa historia baada ya Ubalozi wa Uturiki kupitia taasisi yake ya Diyanet kuwachimbia visima virefu. Visima hivyo viwili vimekabidhiwa kwa Waziri …

Soma zaidi »

WANANCHI CHIBOLI KUFURAHIA SIKUKUU YA EID EL-FITR NA UMEME

Wananchi katika Kijiji cha Chiboli wilayani Chamwino, Jimbo la Mtera, watasherehekea sikukuu ya Eid El-fitr wakiwa na umeme kwa mara ya kwanza, baada ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kuwasha umeme katika Kijiji hicho. Akiwa ameambatana Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga, …

Soma zaidi »

WAZIRI MAKAMBA ARIDHISHWA NA KASI YA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba amefanya ziara ya kikazi ya kukagua viwanda vinavyozalisha mifuko mbadala ikiwa ni siku ya nne tangu kuanza kwa utekelezaji wa Sheria ya Marufuku ya Mifuko ya Plastiki nchini. Akiwa katika Kiwanda Cha African Paper Bag Ltd …

Soma zaidi »