TANESCO KUOKOA MIL. 450 KILA MWEZI BAADA YA KUZIMA MITAMBO YA KUFUA UMEME INAYOTUMIA DIZELI RUVUMA

Screen Shot 2018-09-17 at 10.45.00.png

 Moja ya mitambo ya kufua umeme wa mafuta ya dizeli uliokuwa kwenye kituo cha Songea ikiwa imezimwa.
Kutokana na kuzimwa kwa mitambo ya dizeli iliyokuwa ikitumika kufua umeme kwa matumizi ya mji wa Songea na vitongoji vyake Septemba
13, 2018 baada ya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, Shirika la umeme Tanzania.
Screen Shot 2018-09-17 at 10.45.22.png
TANESCO sasa itaaokoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 450,108,508
zilizokuwa zikitumika kununua dizeli kila mwezi. 
TANESCO iliwasha rasmi kituo kipya na cha kisasa cha kupoza na kusambaza umeme cha Madaba, ambacho kimeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kuondoa matumizi ya umeme wa mafuta kwenye Halmashauri ya Manispaa ya mji wa Songea na vitongoji vyake.
Kuwashwa kwa mtambo huo ni baada ya kukamilika kwa Mradi
wa umeme wa Makambako-Songea ambao ulihusisha ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Makambako na Songea sambamba na upanuzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Makambako, lakini pia  Ujenzi wa njia kuu ya usafirishaji Umeme wa kilovoti 220 yenye urefu wa kilometa 245 kutoka Makambako hadi Songea kupitia Madaba. Usambazaji Umeme wa msongo wa 33kV zenye urefu wa kilomita 900 na kuunganisha wateja 22,700 katika Wilaya za Njombe, Ludewa na mji wa Makambako katika Mkoa wa Njombe, Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbona Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma.
SONGEA 3.png
Screen Shot 2018-09-17 at 10.45.00.png
Tenki la kuhifadhia mafuta ya dizeli, ambalo sasa litabaki kama kumbukumbu, baada ya matumizi yake kukoma rasmi.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

MITAMBO YA KUNYANYULIA MIZIGO YA UJENZI WA MRADI WA JN HPP YAZINDULIWA RASMI FUGA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Atashasta Nditiye amazindua Rasmi Vifaa vya Kunyanyulia Makontena …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *