MIKOA YA DODOMA,GEITA NA NJOMBE YAONGOZA MAKUSANYO YA KIMKOA

MHE. SELEMANI JAFO, WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS - TAMISEMI
Waziri Jafo atangaza Makusanyo ya Halmashauri za Mikoa, Wilaya, miji na majiji.

Waziri Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Selemani Jafo amesema kuwa serikali imekuwa ikifuatilia ukusanyaji wa Mapato katika Halmashauri zote ili kuweza kufanikisha utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri zote nchini.

Waziri Jafo amesema hayo wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya mapato ya Halmashauri zote nchini Mkoani Dodoma.

Ad
  • MAKUSANYO KIMKOA:
  • Amesema kwa upande wa Halmashauri za Mikoa, Mikoa mitatu imekuwa kinara kwa makusanyo ya mapato ya ndani. ameitaja mikoa hiyo ni  Dodoma  ambayo iliyokusanya kwa asilimia 170, ikifuatiwa na Geita iliyokusanya kwa asilimia 104 na Mkoa wa Njombe uliokusanya kwa asilimia 103 ,amesema Mikoa hiyo mitatu ndiyo iliyovuka malengo yake katika ukusanyaji wa mapato.

 

  • Aidha ametaja Mikoa mitatu ambayo ilikusanya kwa asilimia ndogo ni pamoja na mkoa wa  Ruvuma uliokusanya kwa asilimia 46, Simiyu asilimia 59 na Shinyanga asilimia 66
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA mMHE. SELEMANI JAFO
Mhe. Jafo amesema kila Halmashauri ya wilaya itapimwa na kupongezwa (kwa zile zilizovuka kiwango cha ukusanyaji mapato). Hali kadhalika, kwa halmashauri ambazo zimefanya vibaya (chini ya 50% ya kiwango kilichotakiwa kukusanywa), ni lazima itoe maelezo ya kwanini isiuchukuliwe hatua za kiutendaji kwa kushindwa kutimiza lengo.
  • Waziri Jafo amesema kuwa Halmashauri zote zilizokusanya chini ya asilimia 50 ya lengo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 nimezielekezwa kutoa maelezo ni kwanini hazikufikia hata asilimia 50 ya lengo walilojiwekea

 

  •  Ameongeza kuwa mkakati wa makusanyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ni kila Halmashauri katika Mikoa yote isikusanye chini ya asilimia 81 ya lengo lake na kuwaaasa Wakuu wa Mikoa kusimamia mkakati huo katika Mikoa yao.

MAKUSANYO YA MAJIJI KIASILIMIA

Kwa upande upande wa makusanyo ya majiji amesema jiji la Dodoma limekuwa la kwanza katika makusanyo huku jiji la Mbeya likiwa la mwisho katika makusanyo ya majiji.

  • Jiji la Dodoma limekuwa la kwanza kati ya Majiji yote sita ikiwa imekusanya shilingi 25,058,290,000/= kati ya shilingi 19,326,914,686/= sawa na asilimia 130 ya lengo lake wakati Jiji la Mbeyalimekuwa la mwisho kwa kukusanya kiasi cha shilingi 7,836,169,412/= kati ya shilingi 11,010,640,000/= sawa na asilimia 71
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *