TESEApp; Yazinduliwa Rasmi Leo!

TESEApp
Hii ni application mpya nchini Tanzania ambayo imetengenezwa na vijana wa wanasayansi wa Kitanzania. Ni App ambayo imerahisisha mfumo wa ufundishaji na usomaji kwa wanafunzi wa Elimu ya Sekondari nchini.

• Haya ni Matokeo ChanyA+ ya matumizi sahihi ya SIMU ZA MKONONI, TABLETS, LAPTOPS na KOMPUTERS KWA WANAFUNZI WA NCHI YETU!

• Ni ‘application’ inayoweza kupakuliwa (download) katika aina zote za SMART PHONE, TABLETS, LAPTOPS na COMPUTERS.

Ad

 

TESEApp YALIYOMO
App hii ambayo inapatikana katika Taplets maalum pamoja na katika naina zote za simu janja (Smart Phones), Tablet, Laptop na Kopyuta zote; humuwezesha mwanafunzi kufundishwa katika mazingira rafiki kwa kusikiliza huku akitazama mifano na maelezo ya topic za zote za elimu ya Sekondari nchini kisha kumpa nafasi mwanafunzi ya kufanya mazoezi mbalimbali sambamba na kupata usaidizi katika maswali/ topic ambazo hajaelewa.

• Imebuniwa na kutengeneza vijana wazawa, wataalamu wa Kitanzania (Made in Tanzania 🇹🇿)

UZINDUZI WA TESEApp
Uzinduzi wa App hii umefanyika siku ya Jumanne tarehe 09 Septemba, 2018 katika hotel ya SeaShells iliyoko katika jengo la Millenium Tower eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo wadau binafsi wa elimu sambamba na wataalam wa App hiyo waliwaelezea wageni na waandishi wa habari namna ‘application’ hiyo inavyofanya kazi na namna itakavyokuwa msaada baina ya mwalimu na mwanafunzi wa elimu ya sekondari nchini

• Juhudi za Serikali katika kujenga na kukuza sekta ya Elimu nchini zinakuwa kwa kasi na kuleta Matokeo ChanyA+ 110%

• Wataalam waliobuni App hii wanasema hii ni awamu ya kwanza ambayo imekidhi mahitaji ya mwananfunzi wa masomo yote ya elimu ya Sekondari nchini yaani O’level na A’level

MAELEZO KUTOKA KWA MTAALAM KUHUSU TESEApp
Mmoja wa wataalam waliobuni na kutengeneza TESEApp akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali mbele ya waandishi wa habari kuhusu App hiyo mpyA+ na manna itakavyokuwa ikitumika. Anayefuatilia kwa makini pembeni yeke ni mmoja wa maafisa watendaji wa TESEApp

• Wamethibitisha kwamba TESEApp imethibitishwa na Taasisi ya Elimu nchini kuwa na viwango na vigezo zinavyokidhi mahitaji ya wanafunzi wa Tanzania.

UZINDUZI RASMI WA TESEApp

• Vijana hao wataalam wameweza kuwa na aina MpyA+ ya Tablets maalum kwa mwanafunzi ambazo sina notes, materials ya masomo yote ya elimu ya Sekondari Nchini, Masomo ya Dini na mahitaji mengine kwa mwanafunzi nchini.

SOMO LA HESABU NDANI YA TESEApp

• Wadau wa Elimu walioifanyia majaribio TESEApp wamekiri kwamba ni jibu muafaka kwa mzazi kuweza kudhibiti matumizi ya mitandao na Internet kwa watoto wao.

• Pia wamesema App hiyo ni jibu sahihi kwa walimu na wadau wa elimu katika mabadiliko chanyA+ ya kufundishia na mustakabari wa sekta ya elimu kuendana na dunia ya kidogitali.

MAELEKEZO
Kipeperushi cha maelekezo ya yaliyomo na yale ya namna ya kupakuwa (download, kujiunga na kutumia TESEApp kwa mwanafunzi wa elimu ya Sekondari nchini.

• TESEApp inampa uwezo mwanafunzi kusikiliza mafunzo ya walimu kupitia mtandao (kwa SILABASI (TOPICS) ZOTE), kufanya maswali na mazoezi ya silabasi husika, kupata vitabu vya kiada na ziada, kufanya mazoezi ya maswali na mitihani iliyopita (past papers)

SOMOM LA

• TESEApp inarahisisha kazi ya mwalimu na inafupisha mzigo wa kujisomea kwa mwanafunzi na kuokoa muda kwa kuwa na notes zote katika kifaa kimoja.

SPMO LA BAIO
kwani #SisiNiTanzaniaMpyA+ inayopata Matokeo ChanyA+ 110% katika kila nyanja ya kujenga na kukuza uchumi imara na madhubuti kwa Watanzania wote!

Ad

Unaweza kuangalia pia

MWANAFUNZI WA MALANGALI AINGIA KUMI BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

#SisiTumeona SISI WATANZANIA TUNAWEZA Hivi sasa watoto wetu wanapata elimu bure bila malipo! ——————————— Matokeo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *