Hii ni moja ya barabra ambayo haikuwahi kujengwa kwa kiwango cha lami tangu nchi yetu ipate uhuru wake mwaka 1961. Awamu ya Tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaifanya katika kipindi cha miezi 30 pekee ambapo mwezi Aprili kwaka 2020 itakuwa imekamilia.
UJENZI WA BARABARA YA KIDATU – IFAKARA WASHIKA KASI
Ni barabara yenye urefu wa km 66.9 ambayo haikuwahi kujengwa tangu Uhuru, ni moja ya maamuzi ya Serikali ya Awamu ya Tano baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuamua kwa dhati kutekeleza kikamilifu ILANI ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 na ahadi zake wakati wa kampeni za urais.
Mkandarasi tayari ameanza kazi haraka kama agizo la mheshimiwa Rais lilivyomtaka siku ya uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa barabara hiyo
Usafishaji wa eneo itakapojengwa barabara hiyo unaendelea na kilometa nyingi zikisafishwa.
Ujenzi wa barabara hii ya Kidatu – Ifakara kwa kiwango cha lami, unatarajiwa kujengwa kwa miezi 30 na utagharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 111.4 na unafadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (European Union), Shirika la Misaada la Uingereza (UK Aid) na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).