NYERERE DAY: RAIS MAGUFULI NA MKEWE WAMTEMBELEA MAMA MARIA

RAIS MAGUFULI AKISALIMUANA NA MAMA MARIA NYERERE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rai wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Rais Magufuli leo Jumapili tarehe 14 Oktoba, 2018 aliambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli (ambaye hayupo katika picha) na kwenda nyumbani kwa Mama Maria eneo la Msasani jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa ambaye alifariki ratehe 14 Oktoba, 1999.

Katika kuazimisha kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa kilichotokea tarehe 14 Oktoba 1999, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wameshiriki Ibada ya Misa Takatifu maalum ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kanisa la St. Peter Osterbay na kisha kumtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam.

MHE. RAIS AKISALIMIANA NA MAMA MARIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Msasani Jijini Dar es Salaam kumtembelea ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa ambaye pia ni Rais wa Kwanza wa Tanganyoka na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki tarehe 14 Oktoba, 1999.

Ibada hiyo ambayo ilikuwa ikionyesha moja kwa moja na televisheni ya Taifa (TBC1) ilimalizika majira ya saa mbili na kumpa fursa Mhe. Rais kwenda nyumbani kwa Mama Maria kumsalimu kisha kufanya nae mazungumzo.

Ad
MAMA JANETH AKISALIMIANA NA MAMA MARIA
Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere nyumbani kwake alipokuwa akiishi na Baba wa Taifa mtaa wa Msasani kwa Mwalimu jijini Dar es Salaam. Katikati yao, ni Rais Magufuli ambaye aliambatana na Mama Janeth kwenda kumsalimu Mama Maria ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyefariki miaka 19 iliyopita.
WOSIA WA MAMA MARIA
Mama Maria Nyerere akimsimulia jambo Rais John Pombe Magufuli na Mkwe Mama Janeth ambao walimtembelea nyumbani kwake Msasani ikiwa ni katika kuadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa leo tarehe 14 Oktoba, 2018 bikiwa ni miaka 19 baada ya kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Kwanza na Muasisi wa Taifa letu Hayati Dkt, Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Anayefuatilia mazungumzo hayo ni mmoja wa watoto wa Mwalimu Nyerere Ndugu Makongoro Nyerere. Kabla ya kuwasili Msasani kwa Mwalimu, Rais Magufuli na mkewe walishiriki Ibada ya Misa maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa iliyofanyika katika Kanisa la St. Petro Osterbay jijini Dar es Salaam.

 

RAIS AKIMFARIJI MAMA MARIA NYERERE
Rais Magufuli akimfariji Mama Maria Nyerere siku ya Jumapili tarehe 14 Oktoba 2018 ikiwa ni kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarege Nyerere. Mhe. Rais alifika nyumbani kwa Mama Maria kumtembelea baada ya kushiriki misa maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa katika kanisa la St.Petro Osterbay jijini Dar es Salaam ikiwa ni miaka 19 tangu Mwalimu Nyerere alipotutoka. Ibada hiyo ya Misa ya kumuombea Baba wa Taifa ilifanyika katika kanisa hilo ambalo ndilo kanisa alilokuwa akisali Baba wa Taifa enzi za uhai wake.

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AIPONGEZA MAHAKAMA NA WADAU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Rais  Dkt. John  Magufuli ameipongeza Mahakama na wadau wake kwa hatua kubwa za kimaendeleo zilizopigwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *