Serikali Itaendelea Kushirikiana na Kanisa katika Kudumisha Amani na Upendo – Rais Magufuli

Rais Dkt. John  Magufuli akizungumza
Rais Dkt. John Magufuli akizungumza na Waumini mbalimbali wa Kanisa Katoliki, Maaskofu pamoja na Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu mara baada ya Misa iliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani leo
  • Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki hapa nchini kuadhimisha Jubilei ya miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara.
  • Misa Takatifu ya maadhimisho ya Jubilei hiyo ambayo imefanyika Bagamoyo Mkoani Pwani ambako Ukristo uliingia mwaka 1868 imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Nairobi nchini Kenya Mwadhama John Kardinali Njue.

SISI-NI-TANZANIA-MPYA---128

  • Misa hiyo imehudhuriwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, Spika Mstaafu Anne Makinda, Maaskofu wa Majimbo yote ya Kanisa Katoliki hapa nchini na nchi jirani, Mapadre, Watawa na waumini wa Kanisa hilo kutoka majimbo yote hapa nchini.
SISI-NI-TANZANIA-MPYA---125
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Polycarp Kardinali Pengo wapili kutoka kushoto waliokaa, Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinali Njue wapili kutoka
  • Akizungumza katika Misa hiyo, Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Kanisa Katoliki kwa mchango lililoutoa kuwahudumia Watanzania kiroho na kutoa huduma za kijamii tangu miaka 150 iliyopita na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa katika kudumisha amani na upendo na kuwaletea wananchi maendeleo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa kabla ya kuanza kwa Misa takatifu ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  • Rais Magufuli amewashukuru Maaskofu, Mapadre, Watawa na viongozi wote wa Kanisa Katoliki kwa namna wanavyoshirikiana na Serikali na Madhehebu mengine ya dini katika kuleta maendeleo na kuimarisha ustawi wa jamii bila kubagua na amewaomba waendelee kukemea vitendo viovu vikiwemo uvunjifu wa amani, rushwa, ufisadi na ubakaji.
RAIS MAGUFULI AKIWA DINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinal Njue ambaye aliongoza Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  • Aidha, Rais Magufuli amewashukuru wananchi wa Bagamoyo kwa kuupokea Ukristo ambao uwepo wake umeleta manufaa makubwa kwa Watanzania na ameahidi kuwa Serikali itashirikiana na viongozi wa Kanisa hilo kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
RAIS MAGUFULI AKISALIMIANA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinal Njue ambaye aliongoza Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  • Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Gervas Nyaisonga amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuungana na Kanisa Katoliki katika Jubilei hiyo, amempongeza kwa kazi nzuri ya kutimiza ahadi alizozitoa kwa Watanzania katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake na ameahidi kuwa Kanisa Katoliki litaendelea kuliombea Taifa na kushirikiana na Serikali.
Baadhi ya Maaskofu
Baadhi ya Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki wakiwa katika Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AIPONGEZA MAHAKAMA NA WADAU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Rais  Dkt. John  Magufuli ameipongeza Mahakama na wadau wake kwa hatua kubwa za kimaendeleo zilizopigwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *