TANZANIA TUWE WAANGALIFU HISTORIA YA KILIMO IMEJAA HADAA NA HUJUMA TELE

WhatsApp Image 2018-11-22 at 09.03.52(1)

  • Historia ya kilimo duniani inaonyesha jinsi ambavyo mbinu mbalimbali zimetumika kudidimiza kilimo katika nchi zetu Afrika ili tugeuke wategemezi.
  • Hujuma ya kwanza dhidi ya kilimo chetu ilikuwa enzi ya ukoloni, Wakoloni hawakutaka tujitosheleze kwa chakula au tuanzishe viwanda vinavyotumia mazao ya kilimo.
  • Enzi ya ukoloni tulilazimishwa kulima mazao yanayokidhi mahitaji ya viwanda vya wenzetu,ikawa piga ua lazima tulimishwe katani, chai, pamba na kahawa.
  • Baadhi ya wakulima wetu ambao walikaidi kulima mazao hayo wakalima ya chakula waliadhibiwa. Wale waliokubali kulima mazao hayo wakawa ndio wanaohudumiwa na kuitwa ‘Progressive Farmers’.

WhatsApp Image 2018-11-22 at 09.03.52

  • Mazao ya chakula yakapuuzwa sana chini ya ukoloni,reli, barabara na bandari zikajengwa ili kuwezesha mpango wao.
  • Baada ya ukoloni ikaletwa mbinu mpya ambayo inaitwa mapinduzi ya kijani (Green Revolution). Tukafurahia ujio wake sana bila kujua hasa malengo ya green revolution yalikuwa nini. Ikawa kila nchi ya kiafrika imeweka mpango wa mapinduzi ya kijani katika kilimo.
  • Lakini waliokuwa nyuma ya green revolution ni wenye makampuni makubwa ya mbegu, mbolea na viatilifu. Kina Bayer, CIBA Geigy, Sygenta, BASF na wenzao.
  • Hawa nia yao kuu haikuwa kuongeza uzalishaji wa chakula kama walivyokuwa wakidai, nia yao kuu ilikuwa kuongeza soko la bidhaa zao, huo ndio muda zikaanzishwa benki za mbegu.

WhatsApp Image 2018-11-22 at 09.03.53

  • Eneo la SADC ikawekwa pale Lusaka, Mbegu za asili zikafungiwa benki, mbegu za chotara (hybrids) za kina Bayer ndio zikawa zinatamba mashambani.
  • Ni wakati huo sasa vikaanzishwa vituo maalumu vya kuzalisha mbegu chotara kikiwemo kile maarufu kilichopo Las Banos Phillipines kilichokuwa kinazalisha mbegu za mpunga (International Rice Research Centre – IRRI).
  • Nchi zetu za Afrika zikawa watumwa wa haya makampuni kwa mwamvuli wa green Revolution, Nchini India mbegu ya asili ya aina ya BASMATI ikakaribia kutoweka! Baadae ikawekewa hati miliki (patent) ikawa mali ya kampuni.Ikawa marufuku mkulima wa mpunga India kuilima bila idhini au kulipia!
  • Hata baada ya miaka zaidi ya 20 ya Green Revolution bado njaa duniani haikutoweka! Kilichotoweka ni mbegu zetu za asili na uhuru wetu wa kujiamulia tulime nini.

WhatsApp Image 2018-11-22 at 09.04.05

  • Baada ya hadaa ya mapinduzi ya kijani ikaletwa hadaa mpya ya GMseeds. Wengi wanaita GMO! Utaalamu wa GMO unatumika kwenye nyanja nyingi sio mbegu peke yake.
  • Kwa hiyo kwenye mbegu inaitwa GMseeds. Tukaambiwa suluhisho la usalama wa chakula (food security) utapatikana kwa kuhimiza kilimo cha GM seeds. Mabingwa wakiwa kampuni ya Monsato ya US.
  • Ni kweli utaalamu wa GM seeds unaweza kuzalisha chakula kwa wingi kwa kutumia GM seeds au GM tissues, hakika GM tissues inaweza kuzalisha chakula cha kutosha mkoa mzima kwenye chumba chenye ukubwa wa sebule.
  • Lakini pia GM seeds zina uwezo wa kuzaa kwa wingi mashambani, huu ni ukweli usiopingika, lakini kama ilivyokuwa kwa Green Revolution nia sio Food Security. Nia ni ile ile ya kutufanya watumwa wa mbegu na viatilifu vyao.

WhatsApp Image 2018-11-22 at 09.27.56

  • Niwape mifano michache ili mjue GMseeds ni utumwa mamboleo:
  1. Mbegu iliyokuwa genetically modified (GMseed) inaweza kuwa trait-specific. Yaani inakarabatiwa kuwa na sifa maalumu ya kiasili,mfano ili iweze kuzaa itahitaji kiatilifu (kimakosa wengi wanaita dawa) maalumu.Mfano ni mbegu ya mahindi au maharage toka kampuni ya Monsanto,ili iweze kuzaa inakulazimu unyunyuze sumu ya glyphosate’ (inapatikana ndani ya ROUNDUP).Ukijidanganya ukapalilia na jembe la mkono au na sumu nyingine mahindi au maharage yako hayatazaa, ni kwamba ‘kizazi’ cha mahindi au maharage kimetolewa na kuwekwa ndani ya ROUNDUP. Unaponyunyuzia ROUNDUP inafanya kazi mbili: kuua magugu na kubebesha mimba maharage au mahindi yako.Utaalamu huu unaitwa TRAIT SPECIFIC TECHNOLOGY, Maana yake ni kuwa mkulima akishanunua mbegu hii atalazimika kurudi dukani palepale kununua ROUNDUP! Hana ujanja! Huu ndio utumwa mamboleo!
  2. Kuna utaalamu unaitwa TERMINATOR TECHNOLOGY. Mbegu inakarabatiwa inabaki na kizazi kimoja tu (F1 generation). Wengi wanajua hii kupitia mbegu chotara.Ukinunua mbegu chotara itazaa kwa msimu mmoja tu. Msimu wa pili inakulazimu kwenda kununua mbegu tena hata kama umevuna magunia alfu! Utaalamu huu unatumika sana kuzalisha GM seeds.
  3. Utalamu wa Genetic Modification unaweza kutumika kuamua mbegu itakaa muda gani baada ya kuvunwa bila kuharibika au itunzwe kwa njia gani au sumu gani!Yaani ukivuna huna uhuru wa kuiweka muda mrefu hadi bei ipande! Unatakiwa uuze halafu uwahi kununua mbegu kwa msimu ujao.Huna uhuru wa kuihifadhi kwa kutumia majivu au moshi au kwenye kihenge ulichosiriba mavi na mkojo wa ng’ombe! Uamuzi huo unakuwa mikononi mwa kina Monsanto sio mkulima!Mahindi yako lakini wanakuamulia uuze lini na uhifadhi kwa muda gani? Utumwa mamboleo.Tanzania lazima iwe makini sana na hii teknolojia hasa kwenye Mbegu, Ama sivyo kilimo chetu kitakuwa mfukoni mwa kina Monsanto.

WhatsApp Image 2018-11-22 at 09.27.58

  • Hadaa hii ya GMseeds iliambatanishwa na tafsiri potofu ya usalama wa chakula (food security).
  • Kwa mujibu wa United Nation(UN) (kumbuka makampuni haya yana nguvu sana) usalama wa chakula ni KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA.
  • Pia ili eti nchi ijitosheleze kwa chakula lazima iboreshe kilimo kupitia GM seeds na pia chakula cha misaada (food aid).
  • FAO ikapewa kazi ya kupigia debe GM seeds na WFP chakula cha misaada. Dhana hii ni potofu mno.
  • Baadhi yetu tulioshiriki katika UN High Level Task Force on Food Security tuliotoa mawazo yetu kwa nini hii ni dhana potofu.
  • Kwa mfano sisi tulisema kuwa suala si Food Security bali FOOD SOVEREIGNTY.
  • Lazima wakulima wawe na sovereignty katika kuzalisha chakula. Wamiliki ardhi, mbegu, soko, pembejeo na kadhalika.

WhatsApp Image 2018-11-22 at 09.28.00

Kinyume cha hapo ni FOOD COLONIZATION.

  • Pia tulipinga dhana ya kuleta food security kupitia chakula cha misaada. Chakula cha misaada kina madhara yake mengi kwa nchi. Kinaua kilimo cha nchi, kinachochea uvivu, kinatumika kutupa vyakula visivyofaa kwa afya ya binadamu kwenye nchi changa, kinatumika kuingiza GM seeds kinyemela kwenye nchi changa.
  • Kuna nchi chakula cha misaada kimetumika kuhujumu imani za watu. Kuna nchi chakula cha misaada kimetumika kuingiza kwa makusudi GM seeds.
  • Lazima wakulima wetu wawe na food sovereignty ndio tutafanikiwa.
  • Bahati mbaya nchi nyingi za kiafrika ikiwemo Tanzania ziliingia mkenge hadi zikaanzisha wizara za AGRICULTURE AND FOOD SECURITY!
  • Wangeanzisha ‘MINISTRY OF AGRICULTURE AND FOOD SOVEREIGNTY” ndio ingekuwa jibu sahihi kwa hawa wahuni wa kimataifa.
  • Hujuma iliyofuatia ikawa kilimo cha mkataba (CONTRACT FARMING). Hii ndio mbinu iliyotumika kuwaingiza hawa wanunuzi wa mazao yetu ikiwemo korosho.
  • Kilimo hiki kilianzishwa India na Pakistan haswa kwa wakulima wa pamba.
  • Zao la pamba lilianza kupungua sana duniani ikabidi walaji wakubwa wa pamba watunge mbinu ya kujihakikishia udhibiti wa soko la pamba.
  • Ikaonekana wakulima waingizwe kwenye utaratibu wa mikataba. Anakuja mtu anaingia mkataba na mkulima ambao mkulima analazimika kumuuzia mtu huyo zao lake.
  • Kwa kuwa elimu ya wakulima ni ndogo mikataba hii ikawa kiama chao. Mwisho wa msimu mkulima analazimika kumuuzia mtu kwa bei ya kutupa!
  • Akijaribu kumuuzia mwingine mkataba unamzuia hata kama huyo mwingine ana bei nzuri zaidi.
  • Hili ndio linawakuta wakulima wengi nchini. Anadanganyiwa uhakika wa soko kumbe analiwa!
  • Tukitaka kuepuka huu mtego ni kurejesha utaratibu wa mkulima kuuzia serikali kupitia chama cha ushirika. Ushirika ulikuwa kinga ya mkulima. Tatizo ilikuwa ushirika kutowajibika kwa wakulima.

WhatsApp Image 2018-11-22 at 09.27.59

Tatizo lilikuwa kutowajibishana!

Ad
  • Hii haifanyi ushirika usiwe na maana. Turudishe ushirika, tuwape mamlaka wakulima kuwawajibisha watumishi wa ushirika wanapokosea.
  • Tutaachana na hawa walanguzi walioletwa kupitia hadaa ya contract farming.
  • Ni vyema waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia na kuendesha kilimo chetu wakatambua mambo haya ili wasijetumika bila wao kujua kuwaumiza wakulima wetu.

IMEANDALIWA NA Dkt. YAHYA MSANGI(PhD)

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI HASUNGA ATOA SIKU 23 SKIMU YA UMWAGILIAJI NANGANGA WILAYANI RUANGWA KUWA IMEKAMILIKA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa siku 23 pekee kwa wakandarasi wanaojenga Skimu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *