RAIS DKT MAGUFULI NA UHURU KENYATA KUZINDUA KITUO CHA FORODHA CHA PAMOJA Disemba 1, 2018

  • Dkt John Magufuli na Rais Uhuru Kenyata  kesho wanatarajia kuzinduwa
    kituo cha Forodha cha pamoja Namanga One Stop Bonder Point.Aidha Disemba 2,  mwaka huu Rais John Magufuli ataweka jiwe la Msingi la mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh bilioni 520  katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo katika wilaya ya Arumeru.

    Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo alisema kituo hicho cha Forodha kimejengwa kwa ushirikiano wa nchi ya Kenya na Tanzania. Kwa mujibu wa Gambo kituo hicho cha forodha kitakuwa mwarobaini wa kubithibiti vichochoro vya kupitisha magendo zikiwemo nyara za serikali.

 

  • Alisema katika kuimarisha ulinzi wa kituo hicho mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Saimon Sirro ametoa mbwa wawili ambao watagundua aina yeyote ya magendo ikiwemo meno ya tembo,madawa ya kulevya na mlipuko.

    “Niwasihi wananchi wote kuheshimu sheria za nchi kwa kuepuka kufanya vitendo vya kupitisha magendo kwenye mpaka wa Namanga kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimeimarisha ulinzi na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

 

  • Kuhusu uwekaji msingi mradi huo wa maji Gambo alisema Rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi eneo la chanzo cha maji hayo kilichopo wilayani Arumeru.Alisema baada ya kuweka jiwe hilo la Msingi atatembelea ujenzi mradi huo kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha sambamba na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Unaweza kuangalia pia

RAIS MAGUFULI AIPONGEZA MAHAKAMA NA WADAU KWA MAFANIKIO MAKUBWA

Rais  Dkt. John  Magufuli ameipongeza Mahakama na wadau wake kwa hatua kubwa za kimaendeleo zilizopigwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.