Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit (kulia) akifafanua jambo katika kikao hicho huku akisiskilizwa kwa makini na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallaha Ulega na wajumbe wengine hawapo pichani

MISRI YAKUBALIANA NA TANZANIA KUJENGA KIWANDA KIKUBWA CHA NYAMA NA NGOZI

KIWA-1
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akizungumza ofisini kwake baada ya kutembelewa na ujumbe kutoka Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit
  • Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema serikali za Tanzania na Misri zimekubaliana kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha nyama na mazao ya ngozi hapa nchini.
  • Waziri Mpina amebainisha hayo  Februari 5,2019 ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kupata ugeni kutoka nchini Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit.
  • “Tunaenda kujenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama, cha kusindika ngozi, cha kusindika mazao ya ngozi, kiwanda ambacho hakipo katika nchi hizi zote za Afrika ya Mashariki na Kati.” Alisema Mhe. Mpina
  • Waziri Mpina amemuhakikishia waziri huyo wa Misri kuwa rasilimali za mifugo na uvuvi zilizopo nchini zipo salama na kwamba wizara imekuwa ikifanya jitahada kuhakikisha samaki hawavuliwi kwa njia haramu na hakuna biashara haramu ili kuhakikisha rasilimali hizo zinanufaisha viwanda vya ndani na wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta hizo.
  • Aidha Waziri Mpina amemuarifu Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit kuwa hakuna mifugo inayoruhusiwa kuingia nchini kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na vibali na kuwa usimamizi wa nchi katika rasilimali za mifugo na uvuvi uko salama.
  • Katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, makatibu wakuu wa wizara hiyo pamoja na manejimenti ya wizara.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *