SIKU YA WAPENDANAO YA KIPEKEE TANZANIA

TIMOTHEO NA MKEWE SALOME WALIINGIA UKUMBUNI
Bwana Timotheo akiwa amembeba mkewe Bi Salome waliingia katika ukumbi wa Mkapa walimojumuika wapendanao jijini Mbeya kuadhimisha siku ya wapendanao.
  • Imefanyika usiku wa siku ya wapendanao (valentine’s day)
  • Iliandaliwa jijini Mbeya

 

IMG_6629.jpg
Wadau wa siku ya wapendanao waliojumuika jijini Mbeya kusheherekea siku hiyo kwa namna ya kipekee.
  • Ilihusisha viongozi mbali mbali, wakazi wa mkoa wa Mbeya, mikoa jirani sambamba na wapendanao walioongozwa na Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Tulia Akson
MHE DKT. TULIA ACKSON AKIWATAMBULISHA WAGENI MAALUM SIKU YA WAPENDANAO
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwatambulisha wageni maalum wa siku hiyo mbele ya wadau wa siku ya wapendanao. Wageni hao ni familia ya Bwana Timotheo na mkewe Salome. (Kama wanavyoonekana pichani) Bi Salome ni mama mwenye ulemavu ambaye ameolewa na Timotheo ambaye anampenda na aliamua kumuoa licha ya kutambua ulemavu alionao. Baada ya kuoana wamebahatika kupata mtoto mmoja mpaka sasa.

 

  • Waliafikiana kuisaidia ujenzi wa nyumba, malazi, kuwaonyesha upendo familia ya Timotheo na mkewe Salome ambaye ni mwenye ulemavu na ana mtoto mdogo wa miezi kadhaa.
UPENDO WA MFANO WA TIMOTHEO KWA FAMILIA YAKE
Bwana Timotheo akiwa amembeba mkewe Bi Salome na mgongoni amembeba mtoto wao mdogo. Haya ni majumumu ya kawaida kwa Bwana Timotheo awapo nyumbani ambapo husaidia kumuhudumia mkewe sambamba na mtoto wao mchanga.
  • Ni valentine pekee iliyogusa wengi waliohudhuria na kushiriki kuwasaidia wanandoa hao ambao walialikwa kama wageni maalum.
TIMOTHEO NA MKEWE WAKIZUNGUMZA NA WAGENI WAALIKWA
Bi Salome akiwa sambamba na mumewe, akitoa shukrani kwa wadau wa siku ya waopendanao baada ya kualikwa na kuonyeshwa upendo mkubwa siku hiyo.
  • Wote waliohudhuria waafikiana kuendeleza aina hiyo ya usheherekeaji wa siku ya wapendanao na kuwasihi Watanzania wengine kuiga.
SIKU YA WAPENDANAO YA KIHISTORIA TANZANIA
Bwana Timotheo akimbusu mkewe baada ya kumlisha keki. Pembeni yao aliyeshikilia sahani ya keki ni Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson aliyekuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Wapendanao tarehe 14 Februari, 2019 katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.

 

Fuatilia video hii kushuhudia wageni hao maalum walivyoonyeshwa upendo wa kweli siku hiyo

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU AMPONGEZA BONDIA SALIM MTANGO ALIYESHINDA MKANDA WA DUNIA WA UBO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *