MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA CHUO CHA SHYCOM MKOANI SHINYANGA

MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHYCOM mkoani Shinyanga mara baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua ukarabati na ujenzi wa miundombinu.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa haamini macho yake kuona uchafu uliokithiri mara baada ya kutembelea jiko la kupikia chakula cha wanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Taleck (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho John Nandi.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Edward K. Mulumba (kulia) wa Wizara ya Maji yanayohusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ofisi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Shinyanga (KASHWASA)
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHYCOM mkoani Shinyanga mara baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua ukarabati na ujenzi wa miundombinu.
SAMI-5
Picha ya Jengo la Madarasa ya Chuo cha Ualimu SHYCOM ambalo Makamu wa Rais alitembelea na kutaka kujua kwa nini ujenzi wake umesimama. Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga katika ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna kutoka kwa Msanifu wa Pamba Bw. Dotto Ntumba (kushoto) mara baada ya kutembelea maabara ya pamba katika Ofisi ya Bodi ya Pamba mkoani Shinyanga.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna kutoka kwa Msanifu wa Pamba Bi. Sharifa Salum (kushoto) mara baada ya kutembelea maabara ya pamba katika Ofisi ya Bodi ya Pamba mkoani Shinyanga.
WANAFUNZI
Wanafunzi Nchambi Nsile (kulia) anayesoma darasa la 7 akiwa amempakata mwenzake Nyazobe Sembe darasa la 4 wa Shule ya Msingi Jumuishi Buhangija wakati wa kumsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alitembelea shule hiyo na kufungua Bwalo. Makamu wa Rais yupo ziara ya kikazi mkoani Shinyanga.
WANAFUNZI
Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM Happyness Kasuku akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) changamoto ya maktaba ya kusomea ambayo ni ndogo na ina vitabu vichache.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *