SEKTA BINAFSI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI JUU YA MAFUNZO YA KUWAANDAA WATANZANIA KUSHIKA NYADHIFA ZA JUU ZA UONGOZI KATIKA MAKAMPUNI

  • Jukwaa La Taasisi ya Wakurugenzi na wamiliki wa makampuni binafsi Tanzania(CEOrt) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira limekuja na mpango maalum wa kuwawezesha watanzania kushika nyadhifa za juu za Uafisa Mtendaji Mkuu (CEOs) na Ukurugenzi Mtendaji (MDs) katika Makampuni na Taasisi mbalimbali kupitia mafunzo ya kuwajengea uwezo yatakayoratibiwa na Chuo cha Strathmore Business School (SBS).

NAIBU WAZIRI MAVUNDE

  • Hayo yamesemwa jana Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa CEOrt Ndg Sanjay Rughani wakati akijadiliana mpango huo na Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde katika kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kupata mafunzo ili kushika nyadhifa za juu katika Makampuni hasa kutokana na kuonekana kwamba kuna upungufu mkubwa wa watu wenye uwezo wa kushika nafasi hizo kwa sasa ambapo kwa kuanzia juu ya Watanzania 20 wataanza kujengewa uwezo kwa mwaka huu na kuendelea kila mwaka kuongeza idadi.
  • Akizungumza katika kikao hicho,Naibu Waziri Mavunde ameishukuru Taasisi ya CEOrt kwa kuja na mpango wenye tija wa kuijengea uwezo nguvu kazi ya Watanzania ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushika nyadhifa za juu katika makampuni na Taasisi na kuahidi,kwa niaba ya Serikali, kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa Programu hii yenye tija kwa maslahi ya nguvu kazi ya Tanzania.
  • “Hili jambo ni la kizalendo, tunaliunga mkono kama Serikali.Na sisi kupitia Mpango wa Ukuzaji Ujuzi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu tunatekeleza mafunzo ya vitendo (Apprenticeship)  wahitimu wa Vyuo vikuu na Vyuo vya Elimu ya Juu ili kuwajengea uwezo na kuwa na sifa za kuajirika”Alisema Mavunde
Ad

Unaweza kuangalia pia

NAIBU WAZIRI SHONZA: WAZAZI NDIYO WALEZI WA KWANZA WA MTOTO

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wazazi na familia kuwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *