KITUO KIKUBWA CHA BIASHARA CHA AFRIKA MASHARIKI KUJENGWA NYAKANAZI MKOANI KAGERA

 • Serikali inatekeleza mpango mkakati wa kujenga Kituo kikumbwa cha Biashara cha Afrika Mashariki katika eneo la Nyakanazi Mkoani Kagera ili kuwanufaisha wananchi wanozunguka eneo hilo na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki- EAC.
 • Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalaum Mhe. Halima Abdalallah Bulembo, alieuliza kuhusu mpango wa Serikali wa kujenga Kituo cha Biashara katika mkoa wa Kagera unaopakana na nchi nyingi za EAC.
 • Dkt. Kijaji alisema kuwa, ujenzi wa Kituo cha Biashara eneo la Nyakanazi utawezesha wananchi wa Tanzania pamoja na nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda kulifikia soko hilo.
 • Akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo kuhusu mpango wa Serikali wa kuifanya Kagera ifaidike na uchumi wa kijiografia, Dkt. Kijaji alisema kuwa, Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati mkoani humo ukiwemo mradi wa Reli yenye kiwango cha Kimataifa (SGR) kipande cha Isaka- Rusumo chenye urefu wa kilometa 371 na ukarabati wa barabara ya Lusanga- Rusumo yenye urefu wa kilometa 91.
 • Aidha inatekeleza mradi wa umeme wa megawati 80 katika mipaka ya Rusumo na Mtukula kwa ajili ya kuimarisha shughuli za kibiashara na nchi jirani za Rwanda na Uganda.
 • Naibu Waziri Dkt. Kijaji alisema, mazao ya wakulima wa Kagera na bidhaa za baadhi ya viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu vinafaidika kimasoko na jiografia ya Mkoa huo ikiwa ni pamoja na kiwanda cha kusindika minofu ya Samaki cha Fish Co Ltd na Supreme Perch Ltd.
 • Viwanda vingine ni Ambiance Distillers Tanzania Ltd kinachozalisha vinywaji vikali, Bunena Development Co. Ltd, NK Botling Co. Ltd na Kabanga Bottlers Co. Ltd vinavyozalisha maji ya kunywa na kiwanda cha Mayawa kinachosindika wine ya Rosella na juisi.
 • Alisema kuwa, sambamba na utekelezaji wa miradi ya kimkakati, Serikali kupitia Mamlaka ya Biashara (Tan Trade), ilitoa mafunzo ya kuhamasisha kuanzishwa kwa vikundi vya kurasimisha biashara mipakani katika vituo vya Kabanga, Rusumo na Mtukula vinavyopakana na nchi za Burundi, Rwanda na Uganda ili kuwajengea wananchi uwezo wa kutumia fursa za kiuchumi. Na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

9 Maoni

 1. Профессиональные seo https://seo-optimizaciya-kazan.ru услуги для максимизации онлайн-видимости вашего бизнеса. Наши эксперты проведут глубокий анализ сайта, оптимизируют контент и структуру, улучшат технические аспекты и разработают индивидуальные стратегии продвижения.

 2. Mohamed Salah Hamed Mehrez Ghali https://mohamed-salah.liverpool-fr.com Footballeur egyptien, attaquant du club anglais de Liverpool et l’equipe nationale egyptienne. Considere comme l’un des meilleurs joueurs du monde.

 3. Diego Armando Maradona https://diego-maradona.com.az Argentine footballer who played as an attacking midfielder and striker. He played for the clubs Argentinos Juniors, Boca Juniors, Barcelona, ??Napoli, and Sevilla.

 4. Spider-Man https://spiderman.kz the latest news, articles, reviews, dates, spoilers and other latest information. All materials on the topic “Spider-Man”

 5. The fascinating story of the rise of Brazilian prodigy Vinicius Junior https://realmadrid.vinicius-junior-cz.com to the heights of glory as part of the legendary Madrid “Real”

 6. We explore the path of Luka Modric https://realmadrid.luka-modric-cz.com to Real Madrid, from a difficult adaptation to legendary Champions League triumphs and personal awards.

 7. The fascinating story of Marcus Rashford’s ascent https://manchester-united.marcus-rashford-cz.com to glory in the Red Devils: from a young talent to one of the key players of the team.

 8. Analysis of Arsenal’s impressive revival https://arsenal.bukayo-saka.biz under the leadership of Mikel Arteta and the key role of young star Bukayo Saki in the club’s return to the top.

 9. Discover the journey of Charles Leclerc https://ferrari.charles-leclerc-fr.com, from young Monegasque driver to Ferrari Formula 1 leader, from his early years to his main achievements within the team.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *