RC NDIKILO ARIDHISHWA NA UJENZI WA NYUMBA 42 ZA ASKARI MKOANI PWANI AMBAZO ZITAGHARIMU SH.BIL. MOJA

 • Mwnyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, ameridhishwa na ujenzi wa nyumba 42 za askari ambazo zipo kwenye hatua ya umaliziaji kwa kanda maalum ya kipolisi Rufiji na jeshi la polisi mkoani Pwani ambazo zitagharimu sh. bilioni moja.
 • Aidha amewaasa wadau kushiriki kusaidia ujenzi wa makazi ya askari ili kutatua changamoto ya upungufu wa makazi ya askari ilihali kuimarisha ulinzi wa mali ,raia na miradi mikubwa ya kimkakati.
NY 3-01
Mkuu wa Mkoani Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akikagua ujenzi wa nyumba za askari
 • Akizungumza wakati alipokwenda kutembelea ujenzi wa nyumba za askari huko Rufiji, Ndikilo alitaka ujenzi huo ,ukamilike ifikapo Juni 30 mwaka huu, kama amiri jeshi wa majeshi ya ulinzi na usalama ,dkt. John Magufuli alivyoelekeza.
 • Alisema, baadhi ya askari wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa makazi ya kuishi, hali inayosababisha kushindwa kuwahi wakati wakihitajika haraka katika dharula za majukumu yao ya kikazi.
 • “Kutokana na hali hiyo, kwasasa jeshi hilo linajenga nyumba 22 kanda ya kipolisi Rufiji na nyumba 20 za makazi ya askari polisi hao Kibaha mjini ,ambapo kwa mkoa wetu makamanda wa polisi wapo wawili hivyo kila mmoja amekabidhiwa milioni 500 “
 • “Uzuri wa kuanza kuimarisha makazi haya ,mjue mkoa upo karibu pia na mradi mkubwa wa ujenzi wa kuzalisha umeme stigo wilayani Rufiji,kwa maana nyingine maandalizi haya vijana wetu askari tunawaweka tayari na karibu kulinda miradi ya aina hii”alifafanua Ndikilo
 • NY 2-01
  Mkuu wa Mkoani Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo
 • Awali akitoa taarifa fupi juu ya ujenzi unavyoendelea, Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi ambae pia ni kaimu kamanda wa kanda maalum ya kipolisi Rufiji ,Taraja Gibe alibainisha, walipokea milioni 500 ,ujenzi ulianza January mwaka huu ,na wamehusisha wadau mbalimbali ambao wamechangia vifaa na milioni 19.
 • Wakati huo huo kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Wankyo Nyigesa amesema, wamepokea michango mbalimbali kutoka kwa wadau na wawekezaji ambapo jana wamekabidhiwa pia vigae (tiles) kutoka kiwanda cha KEDA kilichopo Chalinze ,zilizogharimu milioni tano.
 • Mkoa wa Pwani ni moja ya mikoa ambayo , Amiri Jeshi wa Majeshi dk. Magufuli akiwa anazindua nyumba za askari polisi mkoani Arusha ,april 7 mwaka 2018, alitoa maelekezo kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) kwamba atapatiwa fedha kwa ajili ya makazi ya askari ,ambapo mkoa huo umeanza utekelezaji baada ya kupokea fungu hilo.na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Ad

Unaweza kuangalia pia

NENDENI MKACHAPE KAZI KWA UADILIFU NA KUTANGULIZA MASLAHI YA TANZANIA – RAIS MAGUFULI

Rais  Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 27 Januari, 2020 amewaapisha Mawaziri 2 na Mabalozi 3 …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *