TANZANIA KUNUFAIKA NA DOLA BILIONI 1.7 KUTOKA BENKI YA DUNIA

 • Uhusiano wa Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania umeimarika baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayesimamia nchi 22 zilizoko Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango kuwa Benki hiyo iko tayari kutoa kwa Tanzania fedha zote za mkopo wa masharti nafuu kiasi cha dola za marekani bilioni 1.7 zilizobaki katika mgao wa 18 wa IDA.
 • Bi. Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi amesema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
KK 2-01
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
 • Alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kutolewa kabla ya kuanza mgao mpya wa 19 wa IDA utakaoanza Julai 2020, baada ya kukamilisha taratibu zote za upatikanaji wa fedha hizo.
 • ”Fedha hizi zitaelekezwa katika kutekeleza miradi kadhaa muhimu ikiwemo ya Elimu, Afya, Mradi wa kusaidia Kaya Masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF, Awamu ya Pili na Uendelezaji wa Miji na Masuala ya Uchumi Jumuishi Visiwani Zanzibar” alisema Bi. Kabagambe

KK 3-01
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), wakifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mkutano kati yao uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Benki hiyo imeahidi kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa kufadhili miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
 • Aidha, alipongeza hatua kubwa zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli, katika kupiga vita rushwa na ufisadi nchini pamoja na kutekeleza miradi ya jamii kwa umahili mkubwa ikiwemo miradi ya kimkakati ya reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa pamoja na mradi wa kufua umeme wa maporomoko ya maji katika mto Rufiji wa Julius Nyerere.
 • Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameiomba Benki hiyo kuisaidia Serikali kwa kuipatia fedha za kufanikisha ujenzi wa miundombinu hiyo ya umeme, reli, maji safi na salama, kuimarisha sekta ya kilimo, viwanda, bandari, rasilimali watu na masuala ya teknolojia ya habari na Mawasiliano-TEHAMA.
KK 4-01
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe, aliye katika ziara ya kikazi hapa nchini, Jijini Dar es Salaam.
 • Alibainisha kuwa miradi hiyo itachochea zaidi ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini wa wananchi kwa kuwa nishati ya umeme itachochea ukuaji wa sekta ya viwanda hivyo na kukuza ajira, wakati reli imara na ya kisasa itaimarisha mtandao wa reli na kuwa uti wa mgongo wa maendeleo ya Tanzania na nchi za Ukanda wa Afrika kwa ujumla.
 • Amepongeza pia uamuzi wa Benki hiyo wa kuruhusu upatikanaji wa fedha kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.7 na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika sekta ya elimu, kusaidia kaya maskini kupitia TASAF, kuendeleza masuala ya uchumi jumuishi Visiwani Zanzibar, masuala ya ardhi na miundombinu ya barabara ili kuboresha shughuli za kiuchumi katika jamii.
KK 5-01
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa pili kulia), akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe, aliye katika ziara ya kikazi hapa nchini, Jijini Dar es Salaam.
 • Akitoa majumuisho ya mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na Mgeni wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban, alisema kuwa Serikali inapongeza uamuzi wa Benki wa kuendelea kuipatia fedha serikali ya Tanzania kwa manufaa ya wananchi.
 • Mpaka sasa, Benki ya Dunia imefadhili miradi 28 ya Maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 5.0 sawa na takriban sh. trilioni 11.5, ambapo miradi 20 ni ya kitaifa yenye thamani ya dola 4.065 bilioni na miradi 8 ni ya kikanda yenye jumla ya dola za Marekani 938 milioni. Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

2 Maoni

 1. Почему теневой плинтус – красивая и практичная деталь интерьера,
  Советы по монтажу теневого плинтуса без дополнительной помощи,
  Как использовать теневой плинтус для создания уникального интерьера,
  Ретро-стиль с использованием теневых плинтусов: идеи для вдохновения,
  Как подобрать цвет теневого плинтуса к отделке стен,
  Теневой плинтус: простое решение для скрытия кабелей и проводов,
  Теневой плинтус с подсветкой: создаем эффектное освещение в интерьере,
  Как сделать помещение завершенным с помощью теневого плинтуса,
  Почему теневой плинтус – важная деталь в оформлении интерьера
  плинтус теневой https://plintus-tenevoj-aljuminievyj-msk.ru/ .

 2. Выбор элитных колясок Tutis, Как выбрать идеальную коляску от Tutis?, Лучшие цветовые решения от Tutis, Секреты долговечности и надежности коляски Tutis, инструкция для новичков, что приобрести для удобства, секреты успешного выбора, Как правильно ухаживать за коляской Tutis?, Почему Tutis – выбор ответственных родителей, Как обеспечить максимальный уют для ребенка в коляске Tutis, полезные советы для удобства, Как выбрать коляску Tutis, подходящую для вашего стиля жизни?, Tutis: инновации и технологии, технологии, делающие коляски лучше, Как подчеркнуть свой стиль с помощью коляски Tutis?, модный атрибут для мам, надежность и комфорт в каждом шаге
  коляска тутис цена коляска тутис цена .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *