Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasili katika Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo,Japan. Katikati ni Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Japan Bw. John Kambona akifuatiwa na Bi. Edda Magembe Afisa Ubalozi. August 26,2019.

WAZIRI WA MAMBO YA NJE PROF. KABUDI ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA ULIOPO TOKYO NCHINI JAPAN

TZ 6-01
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anaingia katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo,Japan. August 26,2019.
  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amewasili jijini Yokohama, Japan tarehe 26 Agosti kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 7 wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development-TICAD 7) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019.
TZ 7-01
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akitoa maelekezo kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Tokyo,Japan Bw. John Kambona akiwa na Afisa Ubalozi Bi. Edda Magembe. August 26,2019.
  • Mkutano huu wa Saba utatanguliwa na kikao cha Maafisa Waandamizi wakiwemo Makatibu Wakuu na Mabalozi tarehe 25 na 26 Agosti 2019 ukifuatiwa na kikao cha Mawaziri tarehe 27 Agosti, 2019 na utahitimiswa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019. Kauli mbiu ya Mkutano huu ni “Kuendeleza Maendeleo ya Afrika kupitia Watu, Teknolojia na Uvumbuzi”.
  • Mkutano wa Saba pamoja na mambo mengine unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano na agenda za kimaendeleo zitakazotelezwa kati ya Japan na Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.
TZ 5-01
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika ofisi ya Balozi wa Tanzania Nchini Japan. August 26,2019.
  • Agenda za mkutano wa mwaka huu zinalenga kujadili mageuzi ya kiuchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kukuza sekta na uvumbuzi. Pia kuimarisha usalama na ustahimilivu endelevu kwenye jamii pamoja na kuendeleza jitihada za kuimarisha amani na usalama barani Afrika. Agenda za Mkutano wa Saba zinaenda sambamba na agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na maazimio mengine ya kimataifa kama Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
TZ 1-01
Baadhi ya wajumbe waliopo Yakohama-Japan kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika 2019 (TICAD7 YOKOHAMA 2019) wakiwa katika kikao kazi cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(hayupo Pichani). August 26,2019.
  • Kutokana na mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya kiuchumi barani Afrika, Mkutano wa TICAD 7 umeandaa ratiba maalum itakayozishirikisha taasisi binafsi na za umma kwenye majadiliano ya kibiashara yatakayofanyika tarehe 29 Agosti 2019. Lengo la majadiliano hayo ni kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Serikali wamiliki wa Kampuni, wafanyabiashara na wawekezaji ili kujadili kwa pamoja masuala mbalimbali ya kukuza baishara, uwekezaji na utalii kati ya Japan na Afrika.
TZ 2-01
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongoza kikao kazi cha ujumbe wa Tanzania uliopo Yakohama Nchini Japan kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika 2019 (TICAD7 YOKOHAMA 2019). August 26,2019.
  • Kadhalika wakati wa mkutano wa saba nchi zote za Afrika zimepatiwa nafasi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali kwa lengo la kutangaza fursa za biashara, uwekezaji na vivutio vya utalii za nchi husika. Tanzania kupitia Bodi ya Utalii (TTB) imejipanga kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini wakati wa mkutano huo.
TZ 3-01
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika ofisi ya Balozi wa Tanzania Nchini Japan. August 26,2019.
  • Mkutano wa Saba wa TICAD utahitimishwa kwa Wakuu wa Nchi kupitisha Azimio la Yokohama na Mpango Kazi wa utekelezaji wa Azimio hilo. Serikali ya Japan ilianzisha jukwaa la majadiliano kati yake na nchi za Afrika mwaka 1993 kwa ajili ya kujadili maendeleo na nchi hizo.
TZ 4-01
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akikagua aina ya vitabu vilivyopo katika Maktaba ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Japan. August,26,2019.
  • Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Ad

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Yokohama, Japan.

26 Agosti 2019

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI ZUNGU AHUDHURIA MKUTANO WA 7 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NA MALIASILI WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI

             

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *