TIC YASAJILI MIRADI 1174, SEKTA YA VIWANDA YAONGOZA UWEKEZAJI

 • Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) katika kipindi cha miaka minne kuanzia Novemba 2015 hadi Novemba 2019, imesajili jumla ya miradi 1174 yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 15,756.9 huku sekta ya viwanda ikiongoza kwa kutoa asilimia 53 ya miradi yote nchini.
 • Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi  Mtendji wa Kituo cha Uwekezaji  Nchini (TIC) Geoffrey Mwambe wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Taasisi hiyo  chini ya Utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.
 • Anaongeza kuwa kati yote iliyosajiliwa nchini, tasnia ya viwanda ina jumla ya miradi 626 huku miradi mahili yenye uwekezaji mkubwa ikiendelea kuwavutia  wawekezaji na kuzidi kuajiri maelfu ya Watanzania pamoja na kusaidia kupunguza uagizaji wa bidhaa na malighafi kutoka nje ya nchi.
 • Aliongeza kuwa kupitia miradi hiyo, jumla ya ajira zipatazo 159,833 zimezalishwa katika ajira za moja huku ajira 60,465 zikizalishwa kutokana na ukuaji wa tasnia ya viwanda nchini na nyingine ikiwemo usafirishaji kutoa ajira (11482), utalii (7861) na huduma nyinginezo (5376).
TIC 1-01
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekazaji nchini (TIC), Bw.Geofrey Mwambe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya TIC kwenye Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.
 • ‘’Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuongeza masoko ya bidhaa zetu za ndani, na tangu dhamira ya uchumi wa viwanda itangazwe na Serikali ya Awamu ya Tano tumeshuhudia ujenzi wa viwanda vingi ikiwemo viwanda vya maziwa katika maeneo mbalimbali ya nchi na sasa hatuagizi maziwa kutoka Uholanzi na jirani zetu nchi ya Kenya kama tulivyokuwa tukifanya huko nyuma’’ alisema Mwambe.
 • Mwambe alisema ili kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kufikia uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda, TIC ilifanya mageuzi na maboresho mbalimbali katika sera na sheria ya uwekezaji Na. 26 ya mwaka 1997 ili kuhakikisha kuwa wawekezaji wa ndani nanje ya nchi wanapata fursa ya kushiriki katika kujenga uchumi.
 • Kwa mujibu wa Mwambe alisema kuwa TIC imeendelea kuimarisha mifumo na taratibu mbalimbali za uwekezaji nchini ambazo awali zilikuwa zikileta usumbufu na vikwazo mbalimbali kwa wawekezaji, ambapo kwa sasa imeweza kuongeza idadi ya watumishi katika ofisi hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa leseni na vibali mbalimbali.
TIC 2-01
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekazaji nchini (TIC), Bw.Geofrey Mwambe akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya TIC kwenye Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Idara ya Habari-MAELEZO, Jijini Dar es Salaam.
 • Akitolea mfano alisema kabla ya kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, TIC ilikuwa na jumla ya watumishi 5 kutoka katika Idara mbalimbali za Serikali lakini kwa sasa kuna jumla ya Maafisa 25 kutoka Wizara, Idara, Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali.
 • ‘TIC tumewaweka pamoja maafisa mbalimbali wa Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Umma kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa leseni na vibali mbalimbali na sasa kuna huduma zote za msingi kwa mwekezaji zinazotolewa moja kwa moja katika dawati letu’’ alisema Mwambe.
 • Akifafanua zaidi Mwambe alisema ndani ya kipindi cha utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano Serikali imeweza kuanzia viwanda vikubwa kupitia miradi ya kimkakati yenye mtaji wa zaidi ya Dola 100- 500 za Marekani ambavyo vimetoa ajira lukuki kwa Watanzania.
 • Akitolea mfano wa kiwanda cha kutengeza vigae ‘tiles’ cha Twyford Ltd kilichopo Chalinze Mkoani Pwani,  Mwambe alisema kiwanda hicho kina mtaji wa kiasi cha Tsh Bilioni 130 kimeweza kutoa ajira za moja kwa moja takribani 2000 ambapo takribani asilimia 90 ya malighafi zake zinazalishwa hapa nchini.
 • ‘Vipo viwanda vikubwa kupitia wawekezaji mahiri ambao wameweza kuwekeza katika miradi mikubwa ya kimkakati nah ii imewezekana kutokana na kufanya mageuzi makubwa ya sera na sharia ya uwekezaji ya mwaka 1997 na sasa uwekezaji wake umeanza kuleta manufaa makubwa nchini’’ alisema Mwambe.
 • Aidha aliwataka wawekezaji pindi wanapopata changamoto mbalimbali wasisite kuwasiliana na ofisi yake kwa kuwa malengo ya ofisi yake ni kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwavutia wawekezaji nchini.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KAIRUKI AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *