BENKI YA BIASHARA NA MAENDELEO MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA YAAHIDI KUTOA FEDHA UJENZI WA RELI YA KISASA

11-01
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, akimpokea Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, jijini Dar es Salaam.
  • Rais na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Admassu Tadesse ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR) kwa kutumia fedha zake za ndani na kuahidi kuwa Benki yake itafanya kila linalowezekana kuhakikisha inatafuta fedha za kujenga reli hiyo
22-01
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, na Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse wakikagua mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha Dar es Salaam – Morogoro, wakiwa wameambatana na Ujumbe kutoka Benki hiyo, Maafisa wa Wizara ya Fedha na Mipango na Watumishi wa TRC, Jijini Dar es Salaam.
  • Dkt. Tadesse ametoa kauli hiyo alipotembelea sehemu ya ujenzi wa miundombinu ya reli hiyo, kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na kujionea kazi kubwa iliyofanyika ambapo amesema mradi huo hautainufaisha Tanzania peke yake bali pia nchi za ukanda wa Afrika hususan ambazo hazipakani na Bahari.
33-01
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, akimuonesha Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse michoro ya Reli ya Kisasa itakavyokuwa baada ya ujenzi kukamilika, alipotembelea Ujenzi wa Mradi huo, sehemu ya kipande cha reli kutoka Dar es Salaam – Morogoro.
  • Kiongozi huyo wa juu wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB) Dkt. Tadesse, ameeleza kuwa mwaka huu Benki yake imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani bilioni moja sawa na takribani sh. za Tanzania trilioni 2.3 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yake mikubwa ya maendeleo.
44-01
Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse akiangalia chuma kilichotumika kutengeneza njia ya treni alipotembelea Ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Jijini Dar es Salaam
  • Ameongeza kuwa Tanzania imenufaika pia na kiasi kingine cha zaidi ya dola za Marekani bilioni moja zilizotolewa na Benki yake miaka ya nyuma na ameelezea kufurahishwa kwake na namna nchi inavyokua kwa kasi kiuchumi na kwamba inakopesheka.
55-01
Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa alipotembelea Ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Jijini Dar es Salaam.
  • Aliahidi kuwa kwa kuwa fedha zinazohitajika kukamilisha ujenzi wa mradi huo wa reli ya kisasa ni nyingi, Benki yake itazishawishi taasisi nyingine za fedha ndani na nje ya Bara la Afrika kuchangia ujenzi huo ili mradi ukamilike kwa wakati ili kuchochea masuala ya Bashara na kuboresha shughuli za usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo.
77-01
Ramani ya picha ya reli itakavyokuwa baada ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), kukamilika
  • Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa, ameishukuru Benki hiyo kwa kuonesha nia ya kusaidia ujenzi wa Reli hiyo katika awamu zinazofuata.
88-01
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), ukiongozwa na Rais wa Benki hiyo Dkt. Admassu Tadesse (wa nne kushoto), Jijini Dar es Salaam.
  • Alisema kuwa mpaka sasa ujenzi wa Reli ya Kisasa ambao umetumia fedha za ndani kati ya Dar es Salaam hadi Morogoro umekamilika kwa asilimia 72 huku kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida kikiwa kimekamilika kwa asilimia 22.
99-01
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bw. Masanja Kadogosa (kushoto) akitoa maelezo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) Rais wa Benki ya Biashara na Maendeleo Mashariki na Kusini mwa Afrika (TDB), Dkt. Admassu Tadesse, alipofanya ziara ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Josephine Majura WFM – DAR ES SALAAM).
  • Bw. Kadogosa amesema kuwa Serikali inatafuta fedha nyingine kwa ajili ya kujenga reli hiyo  kuanzia Makutupora, Tabora, Isaka hadi Mwanza na kwamba watafanya mazungumzo na Benki hiyo kuona namna watakavyofadhili ujenzi huo.Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.