RAIS SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA SOKO LA SAMAKI NA BANDARI YA UVUVI

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Zanzibar imo katika mchakato wa kutekeleza uchumi wa buluu na tayari hatua kubwa zinachukuliwa kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.
  • Rais Dk. Shein aliyasema hayo  katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa soko la samaki na bandari ya uvuvi linalojengwa huko Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja ikiwa ni shamrashamra za sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Z1-01
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiweka jiwe la msingi
  • Alisema kuwa uchumi wa buluu ni chochote kiliopo baharini na katika ufukweni wa bahari ambapo tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imenza kushughulikia uchumi huo na haiko tayari kuachwa nyuma.
  • Alisema kuwa Zanzibar inajiandaa na uchumi wa bahari na tayari imeanzisha Kampuni ya uvuvi ya Zanzibar (ZAFICO), ikiwa ni tayari imeshazindua boti mpya ya uvuvi na nyengine iko njiani inakuja na boti nyengine nne za uvuvi zimeshatengewa fedha zake huku akisisitiza kuwa Kampuni hiyo imejiandaa vizuri sana.
ZZ-01
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu
  • Rais Dk. Shein alisema kuwa Serikali inajenga bandari pamoja na soko huko Malindi ambalo idadi ya wastani ya watu 6000 watafanya kazi katika eneo hilo la soko jambo ambalo litaleta tija sana katika sekta ya uvuvi.
  • Alisema kuwa watu wa Zanzibar wamezungukwa na bahari lakini bahari hiyo haijatumiwa vizuri na badala yake wamekwua wakija watu kutoka nje ya nchi na kuwaiba samaki wa Zanzibar wakiwemo samaki wa jodari.
Ad

Unaweza kuangalia pia

KAMPUNI YA SIGARA TANZANIA(TCC) KUTOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KWA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba utayari wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *