RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI 3 WA BODI

  • Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti 3 watakaoongoza bodi za taasisi 2 za Serikali na 1 ya ubia wa Serikali na Sekta Binafsi.
  • Kwanza, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Gabriel Pascal Malata kuwa Mwenyekiti na Mjumbe wa kuiwakilisha Serikali katika Bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania Ltd.
  • Bw. Malata ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.
  • Pili, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Martha Qorro kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (Institute of Rural Development Planning – IRDP).
  • Prof. Martha Qorro ni Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  • Tatu, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Joseph Rwegasira Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).
  • Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hawa umeanza tarehe 30 Januari, 2020.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *