SERIKALI KULIPA MAFAO YA WALIMU 2631 KABLA YA MWEZI AGOSTI, 2020

Rais Dkt. John Magufuli amesemea kuwa Serikali italipa mafao ya walimu kabla ya mwezi wa Agosti mwaka huu ambapo walimu wanaodai mafao yao ni 2631, amesema hayo katika mkutano wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) uliofanyika mjini Dodoma

“kwa taarifa za jana kutoka mfuko wa PSSSF umepokoea na kulipa trilioni 1.2 kwa walimu wastaafu 15,029 kati ya mwezi Agosti 2018 hadi tarehe 3 Juni 2020 madai yaliyobaki ya walimu 2631 wanaodai bilioni 215 napenda kuwa ahidi hapa kabla ya mwezi Agosti haujafika hawa wote watakuwa wamelipwa fedha zao” Rais Magufuli

Ad

Akizungumzia vipaumbele vya serikali katika sekta ya elimu ni Rais Magufuli amesema kuwa sekta ya elimu inaendelea kuboreshwa na ndio sababu Serikali imebeba jukumu la kugharamia masomo ya shule za msingi na sekondari ambapo toka Desemba 2015 – februari 2020 serikali imetumia trlioni 1.01 kugharamia masomo wanafunzi na kuwaondolea wazazi jukumu hilo.

Aidha, amesema kuwa serikali imeongeza idadi ya shule za msingi kutoka 16,899 mwaka 2015 hadi kufika 17,804 mwaka 2020, kwa upande wa shule za sekondari amesema kuwa idadi ya shule zimeongezeka kutoka 4,708 mwaka 2015 hadi 5,330 mwaka 2020.

Kwa upande wa shule kongwe za sekondari amesema kuwa shule 73 zimekarabatiwa kati ya shule kongwe 89, na kuongeza kuwa mabweni 253 yamejengwa na kuongeza vyumba za mahabara 227 na kupeleka vifaa 2,956 katika maabara hizo.

Rais Magufuli amesema kuwa Serikali pia imeongeza idadi ya madawati kutoka milioni 3 hadi kufikia milioni 8 na hivyo kusaidia kumaliza tatizo la madawati katika shule.

Akizungumzia upande wa vyuo amesema kuwa vyuo 18 vya ualimu vimekarabatiwa na ujenzi wa vyuo viwili vipya vya Mrutuguru na kabaga vimejengwa

Aidha, Amesema Serikali imepeleka komputa 1,550 katika vyuo vyote 35 kwa lengo la kuboresha ufundishaji katika upande wa tehema, Rais Magufuli ameongeza kuwa serikali imeongeza vyuo vya VETA kutoka 672 hadi kufikia 712 mwaka 2020 na kufanya ukarabati na kuboresha vifaa vya kufundishia katika vyuo 54 vya Maendeo ya Wananchi (FDC)

Ad

Unaweza kuangalia pia

HERI YA SIKU YA WAFANYAKAZI, MEI MOSI

Tunawatakia Watanzania wote Heri ya Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi! Ni siku muhimu ya kuenzi …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *