MRADI WA UBORESHAJI WA RELI YA KATI – TIRP DAR ES SALAAM – ISAKA WAFIKA 85%

Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati – TIRP unaogharimu Dola za Kimarekani Milioni 300 upo mbioni kukamilika baada ya mradi huo kufika 85% baada ya kazi kubwa iliyofanyika kati ya Dar es Salaam – Isaka umbali wa Kilometa 970 tangu ulipoanza rasmi utekelezaji wake mwezi Juni 2018. 

Mafundi wakiendelea na kazi ya kukarabati reli


Mradi umelenga kufanya ukarabati wa Reli iliyopo kwa kipande cha Dar es salaam – Isaka ili kuongeza uwezo wa kubeba mzigo toka chini ya Tani 13.5 za uzito wa ekseli hadi tani 18.5 kwa kutandika upya njia za Reli Kilometa 312, kukarabati njia ya reli Kilometa 658, kukarabati makaravati na madaraja 44, kuboresha mfumo wa mawasiliano, kukarabati vituo vya kupakia na kupakua mizigo vya bandari ya Dar es salaam, Ilala na Bandari kavu ya Isaka pamoja na kununua mitambo ya ukarabati wa njia, vichwa vitatu vya treni na Behewa mpya 44 za mizigo, na kukarabati vichwa viwili vya treni. 

Ad
Mafundi wakiendelea na kazi ya kukarabati reli


Mratibu wa mradi wa TIRP Mhandisi Mlemba Singo ameeleza kuwa kwa ujumla maendeleo ya kazi yamefikia 85% huku kazi kubwa inayoendelea kwa kipande cha Dar es Salaam – Kilosa ni kubadilisha Reli na Mataruma kwa kuondoa ya zamani na kuweka mapya pamoja na kuboresha tuta la reli ili viweze kuruhusu kubeba uzito na kwenda mwendokasi iliyopangwa. 


Pia ameongeza kuwa kipande cha Dar es Salaam – Kilosa wako katika hatua za mwisho ambapo takribani  Kilometa 50 kati ya Kilometa 289 ndizo zilizobaki katika kuboresha njia hiyo ya reli na kipande cha kutoka Kilosa hadi Isaka kazi zilizobaki ni chache zikiwemo uwekaji alama za reli, ujenzi wa mitaro na kuhakiki viwango vitakavyoiwezesha treni kwenda mwendokasi wa Kilometa 70 kwa saa. 

Mafundi wakiendelea na kazi ya kukarabati reli

“Kazi hii kwa ujumla itaisha mwezi wa Kumi mwaka huu lakini itaisha kwa vipande, kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Kilosa kazi itaisha mwezi wa kumi lakini kipande cha Kilosa – Isaka kazi itaisha mwezi wa saba” alisema Singo  Mhandisi Singo aliongeza kuwa “Tumeshanunua Behewa 44 za mizigo ziko tayari kwa ajili ya kazi hii, vichwa vinatengenezwa pamoja na kuboresha mfumo wa mawasiliano ambao utawezesha kufungwa Kompyuta katika Stesheni na kuongoza treni kwa kutumia Kompyuta”

Ad

Unaweza kuangalia pia

RAIS SAMIA ATEMBELEA RUKWA.. AANGAZIA AFYA, ELIMU, KILIMO NA MIUNDOMBINU KWA MIRADI YA MAENDELEO.

Katika ziara ya Rais Samia siku ya leo iliangazia kwenye sekta ya Afya, Elimu, Kilimo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *