RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA VIONGOZI 3 WA MKOA WA ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Juni, 2020 ametengua uteuzi wa viongozi 3 wa Mkoa wa Arusha na kufanya uteuzi wa viongozi watakaoshika nyadhifa hizo.

Kwanza, Mhe. Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo na amemteua Bw. Idd Kimanta kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Ad

Kabla ya uteuzi huo Bw. Kimanta alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli itajazwa baadaye.

Pili, Mhe. Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Daqarro na amemteua Bw. Kenan Kihongosi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Kihongosi alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa.

Tatu, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni na amemteua Dkt. John Pima kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Pima alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Bw. Jerry Mwaga kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwaga alikuwa Afisa katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wateule wote wanatakiwa kuwepo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Jumatatu tarehe 22 Juni, 2020 saa 2:30 asubuhi.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Uzinduzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya UCSAF Dodoma: Kuimarisha Mawasiliano Vijijini

25 Aprili 2024, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *