NENDENI MKAZINGATIE VIAPO VYENU – RAIS MAGUFULI

Rais Dkt. John Magufuli amewataka viongozi waliapishwa kuzingatia viapo vyao katika kufanya kazi zao, Rais amesema hayo wakati akimwapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Idd Kimanta aliyemteua hivi karibuni, Ikulu jijini Dar Es Salaam.

Rais amesema kuwa anasikitishwa kuona watu aliowateua, kuwaapisha na kuwaamini kwa niaba ya watanzania hawafanyi kadri ya viapo vyao ”mtakumbuka hivi karibuni Arusha imebidi nitengua uteuzi wa wote niliokuwa nimewateua kuanzia RC, Mkurugenzi wa mji pamoja DC ni kwa sababu katika kipindi karibu cha miaka miwili walikuwa wanagombana tu, kila mmoja ni bosi kila mmoja anatengenza mizengwe ya mwezake sikufurahiswha” amesema Magufuli

Ad

Rais amesema kuwa viongozi hao walifanya kazi zao bila ushirikiano na kutokufanya yale walitakiwa kufanya “sasa nimewateua ninyi sitaki yajitokeze hayo” Amesema Rais Magufuli

Katika uapisho huo Rias Magufili amemuapisha Mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Kimanta, viongozi wengine walioapishwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi, Mkuu wa wilaya ya Monduli Kamishina Msaidizi wa Polisi(ACP) Edward Balele walioapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta.

Wengine ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa aliyeapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morgoro na Bw. Jerry Mwaga Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na Dkt. John Pima Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ambao waliapa kiapo cha maadili

Ad

Unaweza kuangalia pia

Tanzania Yapiga Hatua Kubwa katika Miradi ya Maji, Zaidi ya Miradi 1,500 Yakamilika Vijijini na Mijini.

Tanzania imefanya maendeleo makubwa katika miradi ya maji, na hadi sasa, miradi mingi imekamilika ili …

Oni moja

  1. I like this blog very much, Its a really nice situation to read
    and get information..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *