MCHIMBAJI ALIYEPATA MADINI YA TANZANITE YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 7.8 AMPONGEZWA NA RAIS MAGUFULI

Mchimbaji Bw. Saniniu Laizer (kushoto) akiwa amebeba madini ya Tanzanite amabyo yana jumla ya kilo 15 ambapo jiwe moja lina kilo 9. 2 la thamani ya bilioni 4.5 na lingine kilo 5.8 lenye thamani ya shilingi ya bilioni 3.3 wakati wa tukio la kuuza madini hayo kwa Serikali
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashantu Kijaji  akionyesha madini ya Tanzanite ambayo yamenunuliwa na Serikali kwa thamani ya Shilingi bilioni 7.8 kutoka kwa mchimbaji Bw. Saniniu Laizer
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza wakati wa kukunua Madini ya Tanzanite yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8 kutoka kwa mchimbaji Bw. Saniniu Laizer tukio lililofanyika Wilayani Simajiro Mkoani Manyara.

Rais Dkt. John Magufuli amempongeza mchimbaji mdogo madini Bw. Saniniu Laizer kwa kupata mawe mawili ya Tanzanite yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8 ambayo ameyauza kwa serikali.

Rais Dkt. Magufuli ametoa pongezi hizo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Waziri wa Madini, Doto Biteko ambaye ameongoza zoezi la serikali katika ununuzi wa madini hayo ambayo moja lina kilo 9.2 lenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 na lingine likiwa na kilo 5.8 lenye thamani ya shilingi bilioni 3.3.

Ad

“Na hii ndio faida ya wachimbaji wadogo wadogo na hii ni kudhihirisha kwamba Tanzania sisi ni matajiri kwahiyo nawapongeza sana viongozi, nakupongeza sana wewe Waziri wa Madini, Wizara ya Fedha nampongeza Gavana ,nawapongeza viongozi wa mkoa wa Manyara, Kilimanjaro pamoja Arusha lakini nawapongeza sana wananchi wa Simanjiro kwa kazi nzuri wanazofanya za kujitajirisha” Amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema kuwa Tanzanite hiyo ni kubwa na haijawahi kupatikana maeneo mengine na hivyo kupongeza hatua ya serikali kuamua kununua madini hayo.

Tukio hilo la ununuzi wa Madini hayo limefanyika Wilaya ya Simajiro mkoani Manyara katika kituo cha kuuzia madini, ambapo limehudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashantu Kijaji, Gavana wa Benki Kuu Prof Florens Luoga, Mbunge wa Jimbo la Simanjiro James Millya, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanajro Anna Mghwira na viongozi mbalimbali katika Sekta ya Madini.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Matumizi ya Nishati Mbadala kwa Kupikia na Shughuli Nyingine Zafungua Mustakabali Mpya wa Kimazingira Tanzania

Kutumia nishati mbadala kwa kupikia na shughuli nyingine ni muhimu sana kwa Tanzania kutokana na …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *