MILIONI 780 KUJENGA KLINIKI YA HUDUMA ZA METHADONE MKOA WA TANGA

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaendelea kuboresha huduma za afya nchini ambapo shilingi milioni 780 zimetolewa kwa ajili ya kujenga kliniki ya huduma za methadone kwa waathirika wa madawa ya kulevya mkoani Tanga.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa kituo cha muda cha kutoa tiba ya methadone kwa warahibu wa madawa ya kulevya kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga – Bombo.

Ad

“Kwa kushirikiana na wadau wetu wa maendeleo Mfuko wa Dunia (Global Fund) na Mamlaka ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya tumepata zaidi ya milioni 780 na tumezileta kwa ajili ya kujenga jengo la kutolea huduma ya methadone” amesema Waziri Ummy.

Hata hivyo waziri ummy mwalimu hakusita kuupongeza uongozi wa mkoa wa tanga kwa ubunifu walioufanya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo PEPFAR na Amref -Tanzania, kwa kujenga kituo cha muda kwa ajili ya kutoa tiba kwa warahibu wa madawa ya kulevya ambacho kimegharibu shilingi milioni 20 za Kitanzania.

“Tumeona tunaweza kufanya huduma hizi kwa gharama nafuu, nnafurahi kuona kwamba zimetumika takribani shilingi milioni 20 kwa ajili ya kutengeneza kituo cha muda kwa huduma za kliniki katika Mkoa wa Tanga” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa ilikuwepo haja ya kuwa na kliniki ya methadone kwa Mkoa wa Tanga kutokana na kuwa na waathirika wengi wanaotumia madawa ya kulevya huku mkoa huo ukishika nafasi ya pili ya kuwa nawarahibu wengi wa madawa ya kulevya.

“Mkoa wa Tanga unashika nafasi ya pili ya kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wa madawa ya kulevya, takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha Mkoa wa Tanga una watumiaji taribani 5190 wa madawa ya kulevya” amefafanua Waziri Ummy Mwalimu

Waziri Ummy amesema kuwa hadi sasa kuna kiliniki 8 ambazo zinatoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa Mkoa Wa Dar Es Salaam kliniki hizo zimeanzia katika hospitali ngazi ya mikoa na kushuka chini kwenye hospitali za ngazi ya halmashauri na kutaja maeneo yatakayofuata kuwa na huduma hizo ni pamoja na Bagamoyo, Kigamboni, Mbagala na Tegeta na Magereza ya Segerea.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Haki za Watoto

Tarehe 4 hadi 5 Aprili 2024, umefanyika Mkutano wa Tatu wa Jukwaa la Haki za …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *