MKUTANO WA MAWAZIRI WA KAMATI YA SADC YA ASASI YA USHIRIKIANO WA SIASA, ULINZI NA USALAMA KWA NGAZI YA MAKATIBU WAKUU WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkutano wa Mawaziri wa Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Makatibu Wakuu/ Maafisa Waandamizi umefanyika tarehe 25 Juni,2020, Jijini Dar es Salaam kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing).

Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na baadhi ya Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano huo kwa njia ya Video Conference, jijini Dar es Salaam.

Mhimili wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC unaongozwa na mfumo wa Utatu (Troika) ambapo kwa sasa Mwenyekiti ni Zimbabwe, mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika leo ni maandalizi ya mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 26 Juni 2020 chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Sibusiso Busi Moyo na utakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mambo ya Ndani, Ulinzi na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC.

Ad
Washiriki wakifuatilia mkutano kwa njia ya Video Conference jijini Dar es Salaam

Pamoja na mambo mengine mkutano umepokea na kujadili agenda zinazohusu masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Ukanda wa SADC.Mkutano wa leo umehudhuriwa na nchi wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, DRC,  Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Zambia, Zimbabwe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ni moja ya mihimili ya SADC inayosimamia masuala ya Usirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Kanda. Mhimili huu unatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mkataba wa uanzishwaji wa SADC wa mwaka 1992 na Itifaki ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ya mwaka 2001.

Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI SAME MWANGA KOROGWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati alipotembelea chanzo cha mradi huo eneo la la Nyumba yaMungu Wilaya ya Mwanga wakati akiwa ziarani mkoani Kilimanjaro tarehe 21 Machi 2024. Makamu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *