MAKAMU WA RAIS AZINDUA KITUO CHA RADIO JAMII ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Mboga aina ya Kisamvu inayotengenezwa na Wajasiriamali wa Mkoa wa Kusini Unguja Wakati wa Uzinduzi  wa Kituo cha Redio Jamii Kati FM katika Kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Agosti 12,2020.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaomba wananchi kutumia redio kutoa maoni yenye tija kwa ajili ya kusaidia Serikali ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.  

Makamu wa Rais amesema hayo katika uzinduzi wa Redio Jamii ya Kati FM mradi wa Mpango wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari unaolenga kudhibiti ukatili kwa wanawake na wasichana mjini Zanzibar

Ad

“Naomba nitoe rai kwa UNESCO na waendeshaji wa redio jamii tutakayoizindua na nyingine zote zilizotangulia kuhakikisha kuwa miiko ya kazi ya utangazaji inafuatwa ili kutunza na kuimarisha amani na utulivu wa nchi yetu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wananchi kupitia Redio Jamii Kati FM katika Kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Agosti 12,2020 Baada ya kuzindua rasmi Mradi wa Redio hiyo na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Ni vyema pia mawazo ya makundi yote kwenye jamii ikiwemo wanawake na watu wenye mahitaji maalum yakazingatiwa ili kuhakikisha kuwa redio hii inanufaisha kila mtu katika jamii'” Amesema Makamu wa Rais

Aidha Makamu wa Rais ameagiza kuwa redio zisitumike katika kugawa wananchi bali iwe chachu ya kutoa elimu na kuibua fursa mbali mbali za maendeleo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa kuzindua rasmi Mradi wa Redio Jamii Kati FM na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Agosti 12,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Ad

Unaweza kuangalia pia

Msalaba Mwekundu: Nguzo ya Kibinadamu na Ujenzi wa Jamii Imara

Msalaba Mwekundu, ambao ni sehemu ya Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *