SERIKALI ITAENDELEA KULINDA UHURU WA KUABUDU – RAIS DKT. MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga waumini baada ya kuhudhuria Kilele cha Mkutano Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of GOD (TAG) jijini Dodoma leo Agosti 14, 2020

Rais Dkt. John Magufuli amelipongeza Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) kwa huduma nzuri ya kiroho linayoitoa kwa Waumini wake na kwa mchango wake katika utoaji wa huduma za kijamii kwa Watanzania bila kubagua.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo tarehe 14 Agosti, 2020 alipokuwa akizungumza katika Mkutano Mkuu na Baraza Kuu la Kanisa la TAG lililojumuisha Maaskofu na Wachungaji wa Kanisa hilo wa nchi nzima, waliokutana katika ukumbi wa Chuo cha Biblia Miyuji Jijini Dodoma.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga waumini baada ya kuhudhuria Kilele cha Mkutano Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of GOD (TAG) jijini Dodoma leo Agosti 14, 2020

Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na kusanyiko la Maaskofu na Wachungaji takribani 4,000 waliohudhuria mkutano huo uliodhihirisha uwepo wa Mungu na amewashukuru viongozi hao kwa kazi kubwa wanayoifanya kuliombea Taifa na kutoa huduma za kijamii kupitia shule na vyuo, vituo vya watoto yatima na watoto wa mitaani, miradi ya maendeleo na visima vya maji vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini.

Pamoja na kulipongeza Kanisa la TAG, Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu ambao upo kwa mujibu wa Katiba na itaendelea kutoa ushirikiano katika juhudi mbalimbali za kanisa hilo kuhudumia jamii ikiwemo ujenzi wa Chuo Kikuu Jijini Dodoma ambapo amemuagiza Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge kuhakikisha mpango huo unafanikiwa na uwekezaji mwingine wowote ambao Kanisa hilo litaona inafaa kuufanya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt Barnabas Mtokambali alipohudhuria Kilele cha Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo jijini Dodoma leo Ijumaa Agosti 14, 2020 jijini Dodoma leo Ijumaa Agosti 14, 2020

Katika mkutano huo Askofu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la TAG ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Makanisa ya Assemblies of God Barani Afrika, Dkt. Barnabas Mtokambali amemkabidhi Mhe. Rais Magufuli tuzo ya TAG ya kutambua namna alivyoliongoza Taifa kumtegemea Mungu katika kipindi kigumu cha janga la ugonjwa wa Corona (Covid-19).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt Barnabas Mtokambali alipohudhuria Kilele cha Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo jijini Dodoma leo Ijumaa Agosti 14, 2020 jijini Dodoma leo Ijumaa Agosti 14, 2020

Rais Magufuli amemshukuru Askofu Mkuu Dkt. Mtokambali na Waumini wa Kanisa la TAG kwa tuzo hiyo na ameeleza kuwa Tuzo hiyo inamstahili Mwenyezi Mungu ambaye amesikiliza maombi ya Watanzania na kuepusha madhara ya janga la Corona ambalo limeleta taharuki kubwa duniani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Askofu mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt Barnabas Mtokambali alipohudhuria Kilele cha Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo jijini Dodoma leo Ijumaa Agosti 14, 2020 jijini Dodoma leo Ijumaa Agosti 14, 2020

Pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kwa kuwaongoza Watanzania kumuomba Mungu badala ya kuwafungia watu majumbani, Baba Askofu Mkuu Mtokambali amesema muongozo wa Rais Magufuli wakati wa janga la Corona pia umesaidia kuokoa madhara katika uchumi kutokana na kuwahimiza wananchi kufanya kazi na kuongeza uzalishaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishangilia akiwa meza kuu katika Kilele cha Mkutano Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) jijini Dodoma leo Ijumaa Agosti 14, 2020

Aidha, Rais Magufuli amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania ambapo katika kipindi cha miaka 5 iliyopita imeweza kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa ajili ya Watanzania ikiwemo kuboresha huduma za jamii (afya, maji na elimu) na kujenga miundombinu (barabara, madaraja, umeme, reli na majengo).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu na viongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of GOD (TAG) wakati wa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo jijini Dodoma leo Agosti 14, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika Kilele cha Mkutano Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) jijini Dodoma leo Ijumaa Agosti 14, 2020

Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge railway – SGR) ya Dar es Salaam – Morogoro – Makutupora, kufufua reli ya Kaskazini ya Dar es Salaam – Tanga – Moshi – Arusha, mradi wa ujenzi wa Bwawa la Nyerere kwa ajili ya kuzalisha megawati 2,115 za umeme katika mto Rufiji, usambazji wa umeme vijijini ambao umefikia asilimia 85 na jukumu zito la kuhamisha makao makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of GOD (TAG) baada ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo jijini Dodoma leo Agosti 14, 2020

Kuhusu uchaguzi mkuu, Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wote kushiriki uchaguzi huo kwa amani na utulivu na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwapatia viongozi wenye maono, wachapa kazi na wazalendo kwa Taifa ili wasiangukie kwa viongozi wabadhilifu, wabinafsi ama vibaraka kwa kuwa kazi yao itakuwa ni kubomoa badala ya kujenga.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) katika eneo la Kigongo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *