RAIS MAGUFULI AKAGUA MAGARI YALIYOTAIFISHWA NA AAGIZA YAGAWANYWE SERIKALINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2020 amekagua magari yaliyotaifishwa baada ya kuhusika katika matukio ya uhujumu uchumi, na kisha kuhifadhiwa katika kituo cha mabasi cha zamani Jijini Dodoma.

Sehemu ya magari makubwa na madogo 130 yaliyotaifishwa
baada ya kuhusika katika matukio mbalimbali  ya uhujumu yakiwa
yamehifadhiwa katika  kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma
yaliyokaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli leo Jumanne Agosti 25,  2020

Idadi ya magari hayo ni 130 yakiwemo makubwa na madogo yalikamatwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kisha wahusika kufikishwa Mahakamani na Mahakama kutoa uamuzi wa kuyataifisha.

Ad
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akikagua magari makubwa na madogo 130 yaliyotaifishwa
baada ya kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhujumu yaliyohifadhiwa
kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma leo Jumanne Agosti 25,  2020

Akizungumza baada ya kuyakagua, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Jeshi la Polisi na wote waliohusika kuwakamata waliokuwa wanajihusisha na vitendo hivyo (ikiwemo biashara haramu ya meno ya tembo) na ameagiza magari hayo yagawanywe katika taasisi mbalimbali za Serikali ili yatumike kuendesha shughuli za kuwahudumia wananchi na kuzalisha mali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akikagua magari makubwa na madogo 130 yaliyotaifishwa
baada ya kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhujumu yaliyohifadhiwa
kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma leo Jumanne Agosti 25,  2020

Mhe. Rais Magufuli pia amewapongeza wananchi waliojitokeza kutoa taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watu waliokuwa wanafanya uhalifu kwa kutumia magari hayo na amewaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kukomesha vitendo hivyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akikagua magari makubwa na madogo 130 yaliyotaifishwa
baada ya kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhujumu yaliyohifadhiwa
kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma leo Jumanne Agosti 25,  2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua magari makubwa na madogo 130 yaliyotaifishwa baada ya kuhusika katika matukio mbalimbali ya uhujumu yaliyohifadhiwa kituo cha mabasi cha zamani jijini Dodoma leo Jumanne Agosti 25, 2020
Ad

Unaweza kuangalia pia

“KIPINDI CHA UCHAGUZI TUKIFANYA KAZI ZETU VIZURI NI KIPINDI CHA KUWAELEKEZA WATU”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *