Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora kwa kazi nzuri inayofanywa na Tume hiyo kwa kuweza kutatuwa Changamoto mbalimbali za Wananchi na kuweza kupata Haki zao pale wanapozulumiwa.
Makamu wa Rais amesema hayo leo alipokutana na Ujumbe wa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora uliyoongozwa na Mwenyekiti wa Tume Hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu walipomtembelea kwenye Makazi yake Kilimani Jijini Dodoma.
Aidha Makamu wa Rais ameipongeza Tume hiyo kwa kuweza kubadilika na kufanya kazi vizuri pamoja na kutenda Haki kwa Wananchi na Taasisi zote kwa ujumla.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya haki za Binaadamu na Utawala Bora Jaji Msaafu Mathew Mwaimu ameipongeza Serikali kwa kuweza kuwaletea Wananchi maendeleo Bora na kuitakia kila la heri katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Jaji Mwaimu amesema kuwa Tume yake haipendezewi na vitendo vya baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa ambao wamekuwa wakisema Watu baada ya kunadi Sera za Vyama vyao.