HALMASHAURI YA WILAYA BAHI YAFANIKIWA KUONGEZA MAPATO

Na Zynabu AbdulMasoud,

Halmashauri ya wilaya ya Bahi imefanikiwa kuongeza kipato Cha Wananchi kutoka 420,000 hadi 980,000 na kuongeza mapato ya Halmashauri hadi kufikia sh Bilioni 1.6 kutokana na uwekezaji uliofanywa na serikali ya awamu ya tano kupitia miradi mbalimbali.

Ad

Aidha uwekezaji kwenye sekta ya elimu katika halmashauri hiyo umesaidia kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi kutoka wanafunzi 5,000 mwaka 2015 hadi wanafunzi zaidi ya 10,000 kwa mwaka 2020.

Akizungumza na Amsha Amsha ya Uhuru Fm iliyoingia siku ya pili,mkurugenzi wa halmashauri ya Bahi Dkt Fatma Mganga amesema usajili wa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza umeongezeka kutoka wanafunzi zaidi ya 1,000 mwaka 2015 hadi wanafunzi 2,700 kwa mwaka 2020.

“Miradi ya kimkakati imetekelezwa kwa asilimia 90,madarasa 700 yameongezwa kuendana na ongezeko la wanafunzi kupitia Mpango wa Elimu bila ya malipo,tumekarabati majosho sita ya mifugo na hivyo kupunguza vifo vya mifugo,”alisema.

Amesema uamuzi wa serikali kuhamisha Makao Makuu ya Dodoma wananchi wamenufaika kupitia Soko la Mchele na Nyama na kutaja mipango ya Halmashauri ya baadae kuwa ni kuanzisha kiwanda cha ngozi.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya hiyo Mwanahamisi Munkunda amesema mwaka 2015 vijiji vilivyounganishwa umeme vilikuwa sita laki hadi Sasa wamefanikiwa kuunganisha umeme katika vijiji 42 kati ya vijiji 59 vilivyopo ambapo dhamira ni kuunganisha vijiji vyote vilivyobaki mwaka huu.

“Suala ya vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo katika awamu ya Pili tulipokea 45,000 na tumevigawa Ili kuwezesha wafanyabiashara hao kufanya shughuli zao katika mazingira rafiki,”alisema.

Wakizungumza na Amsha Amsha wakazi wa Bahi wamemtaja Rais Dkt John Magufuli kuwa shujaa na mkombozi wao.

“Mimi maisha yangu yalikuwa duni,lakini kupitia mkopo unaotolewa na halmashauri kwa akina mama nimeweza kukopa na kufanya biashara ya kuku hivi sasa naweza kuendesha familia yangu,namshukuru sana,Mwenyezi Mungu ampe maisha marefu Ili afanye Mambo mengine zaidi,”amesema Silivia Chishomi mkazi wa Bahi.

Wilaya ya Bahi ina wakazi 271,069 na wakazi wa wilaya hiyo wanasifika kwa kilimo cha mpunga na ufugaji.

Ad

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Bw. Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *