Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya China Wu Yi kukamilisha ujenzi wa Daraja la Mto Koga lenye urefu wa mita 120 ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu na kuruhusu magari kupita juu yake badala ya kutumia daraja la zamani.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kukamilika mapema kwa ujenzi wa barabara ya Tabora – Koga – Mpanda (km 342.7), kwa kiwango cha lami kwani itaongeza uchumi wa wananchi na kuongezeka kwa shughuli za kibiashara kwa kuwa ni mikoa yenye uzalishaji mwingi wa bidhaa za kilimo.