Taarifa Vyombo vya Habari

SIMBACHAWENE APONGEZA JUHUDI ZA UTUNZAJI MAZINGIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene amepongeza juhudi za utunzaji wa mazingira zinazofanywa na wadau mbalimbali hapa nchini. Simbachawene ametoa pongezi hizo kwa wadau Katibu Mtendaji wa asasi ya Foundation for ASM Development (FADev) Bibi Theonestina Mwasha na Emmanuel Chisna waliofika ofisini kwake …

Soma zaidi »

DKT. MPANGO: WAHASIBU MAFISADI KUKIONA CHA MOTO

Waziri wa Fedha na Mipango  Dkt. Philip Isdor Mpango, ameiagiza Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wahasibu wote wanaofanya vitendo vinavyokinzana na maadili ya kitaaluma ya uhasibu kama wizi, ubadhirifu wa mali za umma, ufisadi na rushwa. Dkt. Mpango alitoa maagizo hayo wakati akifungua …

Soma zaidi »

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUENDELEZA MIRADI YA MAJI SAFI NA SALAMA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya juhudi kubwa katika kuendeleza miradi ya maji safi na salama na si muda mrefu changamoto ya upatikanaji huduma hiyo itakuwa ni historia. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake wakati wa ufunguzi …

Soma zaidi »

RAIS DKT. SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA JENGO LA MICHEZANI MALL NA JENGO LA SHEIKH THABIT KOMBO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa kulikuwa kuna kila sababu ya kufanyika Mapinduzi matukufu ya Januri 12, 1964 ili kuleta usawa na umoja sambamba na kuwafanya Waafrika waishi maisha bora. Rais Dk. Shein aliyasema hayo  katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla …

Soma zaidi »

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa ardhi iliyotengwa kwa ajili ya kilimo hapa Zanzibar ni vyema ikatumika kwa ajili ya shughuli hiyo na si vyenginevyo. Rais Dk. Shein aliyasema hayo  katika hotuba yake aliyoitoa katika uwekaji wa jiwe la msingi la …

Soma zaidi »

RAIS SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA SOKO LA SAMAKI NA BANDARI YA UVUVI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Zanzibar imo katika mchakato wa kutekeleza uchumi wa buluu na tayari hatua kubwa zinachukuliwa kuhakikisha lengo hilo linafikiwa. Rais Dk. Shein aliyasema hayo  katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi …

Soma zaidi »

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA WA 2019 IMEOKOA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 28 KWA KUFANYA UPASUAJI WA MOYO KWA WAGONJWA 1873

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha mwaka mmoja  wa 2019 imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 28 kwa kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 1873 . Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma za matibabu …

Soma zaidi »

RAIS MAGUFULI ATOA WITO KWA WATANZANIA KUANZISHA BUSTANI ZA WANYAMA

Rais Dkt. John  Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wengi zaidi kujitokeza kufuga wanyamapori kupitia bustani za wanyama (Zoo), ili kuongeza idadi ya wanyama hao na hivyo kupanua fursa za utalii na ajira. Rais Magufuli amewapongeza baadhi ya Watanzania walioanzisha Zoo hizo wakiwemo Lut. Jen Mstaafu Samwel Ndomba (Lugari Mini Zoo …

Soma zaidi »