SIMBACHAWENE APONGEZA JUHUDI ZA UTUNZAJI MAZINGIRA

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), George Simbachawene amepongeza juhudi za utunzaji wa mazingira zinazofanywa na wadau mbalimbali hapa nchini.
  • Simbachawene ametoa pongezi hizo kwa wadau Katibu Mtendaji wa asasi ya Foundation for ASM Development (FADev) Bibi Theonestina Mwasha na Emmanuel Chisna waliofika ofisini kwake kuwasilisha maelezo ya michango yao kuhusu masuala ya utunzaji mazingira.
M4-01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) George Simbachawene akipena mikono na Katibu Mtendaji wa asasi ya Foundation for ASM Development (FADev) Bibi Theonestina Mwasha mara baada ya kumalizika kwa kikao.
  • Alisema kuwa wadau hao ni mfano mzuri wa kuigwa kwani na wananchi wengine ambapo alihidi Serikali iko tayari kushirikiana nao bega kwa bega katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa.
  • “Tunatambua juhudi zenu wote katika masuala mazima ya utunzaji wa mazingira na sisi kama Ofisi ya Makamu wa Rais tutaendelea kuhamasish wananchi waendelee kupanda mti na kuitunza,” alisema.
  • Waziri huyo aliongeza kwa kusisitiza kuwa kila mkoa na wilaya hapa nchini umewekewa malengo ya kufikia katika zoezi upandaji wa miti kupitia wananchi wa maeneo yao.

M5-01
Mdau wa mazingira kutoka jijini Dodoma, Emmanuel Chisna akitoa maoni kuhusu umuhimu wa utunzaji mazingira katika kuboresha Jiji la Dodoma na mchango wa utunzaji mazingira katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.
  • Kwa upande wake Bibi Mwasha alisema kuwa asasi hiyo ni inaunga mkono juhudi za kupunguza matumizi ya kemikali ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu ambayo yanatajwa kuwa na athari kwenye afya na mazingira kwa ujumla.
  • Alisema kuwa katika kipindi cha utekelezaji wa shughuli za asasi hiyo wameanzisha migodi darasa mkoani Geita ambayo inatumika katika kutoa elimu kwa wachimbaji hao kuhusu namna nzuri ya kushiriki katika shughuli za kutunza mazingira.

    Ad

  • Katibu mtendaji huyo aliongeza kuwa madhumuni yao ni kuhamasisha urasimashaji migodi yao, kuhakikisha sheria inafuatwa na kutyoa hamasa kwa wanawake katika kushiriki uchimbaji akisema kuwa hawafaidiki sana na shughuli hizo.

M2-01
Katibu Mtendaji wa asasi ya Foundation for ASM Development (FADev) Bibi Theonestina Mwasha akitoa maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na asasi hiyo kuhusu mazingira kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. George Simbachawene na watendaji kutoka Idara ya Mazingira wa Ofisi hiyo.
  • Nae mdau wa mazingira kutoka Dodoma, Chisna Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ifadhili miradi ya majiko banifu na yenye kutumia nishati mbadala ili wananchi waweze kuyapata kwa bei nafuu.
  • “Mheshimiwa waziri haya majiko banifu niliyotaja hapo awali ni rafiki wa mazingira pia yatasaidia kunusuru uoto wa asili unaoendelea kushambuliwa na wananchi wanaotafuta kuni na mkaa,” alisema.
M3 -01
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  George Simbachawene akimpongeza mdau wa mazingira kutoka jijini Dodoma, Emmanuel Chisna baada ya kumalizika kwa kikao
  • Aidha, alishauri Serikali za vijiji na mitaa kwa uangalizi wa halmashauri za wilaya kuwasimamia wananchi kupanda miti ya kivuli kuzunguka nyumba zao angalau miti 10 kwa kila kaya za vijijini akisema itasaidia kutunza mazingira.
  • Mdau huyo alifafanua kuwa miti itakayopandwa inaweza kutumika kama kuni kupitia kupogolea matawi ya miti hiyo. Serikali inaweza kufadhili miche ili wananchi waweze kupata miche ya kutosha na iliyoandaliwa kitaalamu.

 

Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *