SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUENDELEZA MIRADI YA MAJI SAFI NA SALAMA

  • Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inafanya juhudi kubwa katika kuendeleza miradi ya maji safi na salama na si muda mrefu changamoto ya upatikanaji huduma hiyo itakuwa ni historia.
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Mkoa wa Mjini Magharibi (ZUWSP)-ADF 12 huko Saateni Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni shamrashamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

ZZ1-01

  • Rais Dk. Shein alisema kuwa Awamu ya Saba imeanza mikakati kabambe ya kuimarisha miradi ya maji na kueleza kuwa Awamu zijazo zitaendeleza mikakati hiyo kwa azma ya kuwapatia wananchi huduma hiyo muhimu hapa nchini.
  • Rais Dk. Shein alisema kuwa huduma za maji safi na salama kabla ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 zilikuwa zikitolewa kwa ubaguzi licha ya kuwa ni neema aliyoileta MwenyeziMungu kwa waja wake.
  • Alisema kuwa kwa Zanzibar wakati huo huduma zote muhimu zilianza katika nyumba za mawe zilizokuwepo katika eneo la Mji Mkongwe pekee yake.

ZZ2-01

  • Rais Dk. Shein alieleza umuhimu wa maji kwa wanaadamu, wanyama na miti na kueleza kuwa ndio maana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikafanya juhudi za makusudi kuhakikisha huduma hiyo inaimarika hasa ikizingatiwa kuwa maji hayana mbadala.
  • Aidha, Rais Dk. Shein alieleza jinsi ya Washirika wa Maendeleo wakiwemo nchi rafiki ikiwemo Ras al Khaimah, Sharja, Japan, China, India na wengineo walivyoiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha miradi ya maji safi na salama hapa nchini
Ad

Unaweza kuangalia pia

KAMPUNI YA SIGARA TANZANIA(TCC) KUTOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI KWA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba utayari wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.