Taarifa Vyombo vya Habari

OCP NA ETG YAAGIZWA KUWA NA MAGHALA YA KUIFADHIA MBOLEA KUFIKIA JULAI 2019

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeyaagiza makampuni ya Premium Agrochem, OCP na Export Trading Group (ETG) kuhakikisha kwamba ifikapo Julai, 2019 kampuni hizo ziwe na ghala za kuhifadhia mbolea na mawakala wa kusambaza katika mikoa inayotumia mbolea kwa wingi ukiwemo mkoa wa Katavi ili kuondoa changamoto ya upungufu wa mbolea kwa wakulima katika maeneo …

Soma zaidi »

KAZI YA KUSIMIKA MIFUMO NDANI YA TERMINAL III IMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 96.8

Tanzania mpya imedhihirishwa na Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal 3)  katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Akizungumza na Idara ya Habari Maelezo hivi karibuni Msimamizi wa mradi  wa ujenzi wa uwanja huo kutoka Wakala wa Taifa wa Barabara TANROADS, Mhandisi Barton Komba amesema: …

Soma zaidi »

HOSPITALI KUBWA YA KIJESHI YA KIWANGO CHA ”LEVEL 4” KUJENGWA MKOANI DODOMA

Serikali ya Shirikisho la Ujerumani kupitia Mpango wa Kusaidia Majeshi Rafiki imekubali kuongeza kipindi cha kutoa misaada kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa miaka 4 zaidi kuanzia mwaka 2021 hadi 2024 ambapo pamoja na mambo mengine itajenga Hospitali kubwa ya Kijeshi yenye kiwango cha “Level 4” …

Soma zaidi »

DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUENDELEZA MIRADI YA UMEME VIJIJINI

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuendelea kusambaza umeme vijijini mara wakandarasi wa umeme vijijini wanapomaliza kazi kwa mujibu wa mkataba. Dkt. Kalemani aliyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini katika Wilaya za Mpwapwa na Bahi mkoani Dodoma ambapo aliambatana …

Soma zaidi »

SERIKALI KUWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU UN

Katika kutekeleza ajenda za Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s), Serikali imejipanga kuwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Hiari (VNR) katika Jukwaa la Siasa la Umoja wa Mataifa (HLPF) mwezi Julai mwaka huu mjini Newyork nchini Marekani. Hayo yameelezwa na  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera), Bw. Adolf  Ndunguru wakati …

Soma zaidi »